ROSE MUHANDO ATAMANI KUHAMIA KWA GWAJIMA

NYOTA wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando amesema anatamani sana kuhamia kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima kutokana na mahubiri yake mazuri.
Nyota wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
“Natamani nihamie katika kanisa la Mchungaji Gwajima lakini mimi huwa napenda kumuita Askofu kwa sababu ya upako alionao, naomba ikiwezekana na mimi nihamie hapa,” alisema Rose.
Mchungaji Gwajima.
Katika siku ambayo kulikuwa na sala ya shukurani kanisani kwa Gwajima Jumapili iliyopita Kawe jijini Dar es Salaam,  mchungaji huyo alimwambia Rose aliyealikwa kuimba, kwamba yupo tayari kumjengea kanisa Dodoma anakoishi na yeye mwenyewe alisimamie.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger