Showing posts with label ROSE NDAUKA. Show all posts
Showing posts with label ROSE NDAUKA. Show all posts

ROSE NDAUKA ASEMA UCHUMBA WAKE NI NGANGARI KINOMA

MWIGIZAJI nyota wa filamu, Rose Ndauka ameibuka na kukanusha vikali uvumi uliozagaa kuwa uchumba wake na Malick Bandawe umevunjika na kusema siyo kweli kwani bado upo ngangari kuliko kawaida.
Mwigizaji nyota wa filamu Bongo, Rose Ndauka akipopzi.
Akistorisha na gazeti hili juzikati, mwigizaji huyo anayeishi na mchumba wake huyo, alisema uvumi huo hauna msingi kwa sababu asubuhi ya siku hiyo (Jumatatu) alikuwa amemnyooshea nguo alizovaa wakati akielekea kazini kwake.
Rose Ndauka akiwa na mpenzi wake Malick Bandawe.
Awali, kulikuwa na madai ya kuwepo kwa mtafaruku baina ya wawili hao na kudaiwa kuachana kutokana na mmojawapo kulala nje siku tatu, kitendo kilichochochewa na kuonekana kwa Rose akiwa peke yake wakati wa fainali za kumtafuta msanii chipukizi zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City wiki iliyopita.
Read more >>

ROSE MUHANDO ATAMANI KUHAMIA KWA GWAJIMA

NYOTA wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando amesema anatamani sana kuhamia kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima kutokana na mahubiri yake mazuri.
Nyota wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.
“Natamani nihamie katika kanisa la Mchungaji Gwajima lakini mimi huwa napenda kumuita Askofu kwa sababu ya upako alionao, naomba ikiwezekana na mimi nihamie hapa,” alisema Rose.
Mchungaji Gwajima.
Katika siku ambayo kulikuwa na sala ya shukurani kanisani kwa Gwajima Jumapili iliyopita Kawe jijini Dar es Salaam,  mchungaji huyo alimwambia Rose aliyealikwa kuimba, kwamba yupo tayari kumjengea kanisa Dodoma anakoishi na yeye mwenyewe alisimamie.
Read more >>

ROSE NDAUKA :NAISHI VIZURI KWA VILE SIENDEKEZI MAKUNDI YA KIJINGA

MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka ameweka wazi kwamba kinachomfanya aishi vizuri na wenzake ni kutoendekeza makundi.
Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Rose Ndauka.
Akipiga stori na mwandishi wa gazeti hili, Rose alisema anampenda na atampenda mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa na urafiki naye kwa sababu hiyo ndiyo staili yake ambayo inamfanya hata wanaomchukia katika makundi hayo wampende.
“Nampenda kila mtu na nipo tayari kuwa na urafiki na mtu yeyote atakayekuwa tayari kuwa karibu na mimi, makundi hayana maana kabisa zaidi ya majungu tu,” alisema Rose.
Read more >>

ROSE NDAUKA NA CHAZ BABA BIFU ZITO, SOMA ZAIDI HAPA

TIFU! Ni dhahiri kuwa sasa, staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka na Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ wapo kwenye bifu zito.Habari kutoka kwa chanzo chetu zinasema kuwa, chanzo cha bifu hilo ni fedha, ambapo Rose alikodisha gari la Chaz Baba kwa ajili ya matumizi yake lakini akalirudisha likiwa limeharibika na kumuomba Chaz alitengeneze kisha angemlipa fedha zake, lakini hakufanya hivyo.
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka
“Alikodi gari kwa Chaz, lakini aliporudisha lilikuwa bovu, akamuomba Chaz alitengeze angemlipa, baada ya hapo akaingia mitini. Chaz alikasirika sana, maana hata Rose alipopigiwa simu alikuwa hapokei.
“Imefikia hatua Chaz ametoa kiapo kibaya, amesema hata akifa, maiti yake isizikwe mpaka Rose alipe fedha zake kwanza,” kilitiririka chanzo hicho.

Akizungumzia ishu hiyo, Chaz alisema, kitu alichokifanya Rose si kizuri na kamwe hawezi kumsamehe mpaka amlipe fedha zake.
Huyu hapa anafafanua zaidi: “Unajua Rose alikuja kwangu na kukodi gari yangu aina ya Toyota Noah, akarudisha likiwa halitamaniki kabisa, nilipomwuliza akasema walipata ajali, nikamtaka akalitengeneze, akasema hana pesa kwa hiyo nitengeneze atanilipa.
Rais wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’
“Tangu siku hiyo sijaona simu yake wala meseji, hata nikimpigia hapokei. Nimeingia hasara ya kwenda kutengeneza kwa shilingi laki tano, pesa yangu inaniuma, nataka anilipe.
“Hata kama nikifa leo, maiti yangu isizikwe mpaka Rose alipe haki yangu kwanza. Akitangulia yeye utaratibu utakuwa hivyo sitokubali azikwe hadi ndugu zake wanilipe fedha zangu,” alisema Chaz Baba.
Baada ya kupata habari hiyo Risasi Jumamosi lilimhoji Rose kulikoni ameshindwa kulipa deni la watu hadi mdai anatoa kiapo kibaya kama kile, akaruka vikali.

“Ni kweli kabisa mimi nilikodi gari ya Chaz nikawa natembelea na ilivyokuja kuharibika nililitengeneza mimi na kwenda kumkabidhi lakini hakuridhika na namna lilivyotengenezwa  ndiyo maana anasema ananidai lakini mimi sijui hilo deni,” alisema Rose.
Read more >>

NDOA YA ROSE NDAUKA HATIHATI KUVUNJIKA

Staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka akiwa na familia yake.
Cherekochereko! Baada ya maswali ya muda mrefu na kwamba ndoa hakuna, hatimaye mipango kabambe ya ndoa ya staa wa sinema za Kibongo, Rose Donatus Ndauka na mchumba’ke, Malick Bandawe imekamilika ambapo sasa siku zinahesabika.
Kwa mujibu wa Malick ambaye pia ni msanii, kulikuwa na maandalizi ambayo yalikuwa yakiendelea hivyo kwa sasa kila kitu kipo sawa na kinachosubiriwa ni kugawa kadi ambazo zitakuwa zinaonesha tarehe ya ndoa.
“Sasa hivi dogo amekua, anaweza kufanya fujo mbili-tatu hivyo kinachofuata ni ndoa, kadi zitaanza kugawanywa soon,” alisema Malick ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyezaa na Rose Ndauka
Read more >>

ROSE NDAUKA AMKIMBIA HAWARA WAKE, KISA MFUNGO

Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka hivi karibuni aliamua kumkimbia mumewe Malick Bandawe, kisa mfungo wa Ramadhani ambapo sasa anaishi Kigogo na mama yake mzazi.
Staa wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka katika pozi.
Akipiga stori na Ijumaa, Rose alisema amelazimika kwenda nyumbani kwao ili kumpisha mumewe atimize nguzo hiyo ya Uislam bila kipingamizi kutokana na kutokufunga ndoa.
Rose Ndauka akiwa na Malick Bandawe 
“Mimi sifungi hivyo nimeona pia ni jambo la busara kumpa nafasi mwenzangu kwa ajili ya kufanya ibada hiyo, mwezi ukiisha nitarudi na maisha yetu yataendelea kama kawaida,” alisema Rose ambaye awali alikuwa akiishi na mumewe huyo Tandale jijini Dar.
Read more >>

ROSE NDAUKA: TUMEMALIZA BIFU NA JACK CHUZ, SASA KAZI TU!


STAA wa filamu Bongo, Rose Ndauka  amefunguka kuwa kwa sasa yeye na msanii mwenzake, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’  ambaye aliwahi kukwaruzana naye wameshamaliza na kujikita katika kazi zaidi.
Staa wa filamu Bongo, Rose Ndauka.
Akichonga na paparazi wetu, Rose alisema wamerudi kwa staili ya tofauti kwani kila mmoja anafanya kazi zake lakini wanashirikishana na wana ‘project’ maalum ambayo wataifanya hivi karibuni.
“Mimi na Jack kwa sasa tunafanya kazi hata Wema ambaye tulikuwa naye kwenye kundi moja tukiwa na filamu ya kumshirikisha tutamuita kwa sababu hatuna kinyongo kwani bifu hazijengi kikubwa tunafanya kazi tu,” alisema Rose.
Staa wa filamu Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ kulia akiwa na Rose Ndauka.
Rose na Jack Chuz walipishana kipindi cha nyuma na chanzo kikidaiwa kuwa ni kuibiana mabwana lakini hivi karibuni walimaliza tofauti ambapo walionekana pamoja kwenye msiba wa aliyekuwa muongozaji wa filamu nchini, George Otieno ‘Tyson’.
Read more >>

ROSE NDAUKA AFUNGUA ALIVYOWAMWAGA WANAUME NA KUTULIA NA MALIKI

AMA kawa, leo katika Exclusive Interview tunaye mwigizaji Rose Ndauka ambaye anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni.Kwenye maisha yake ya sanaa, amepitia mambo mengi ambayo yanasisimua, katika makala haya utayapata kwa ukamilifu wake:

Mwigizaji maarufu wa filamu za kibongo Rose Ndauka akiwa na mumewe Maliki
ALIVYOANZA KUIGIZA
Ilikuwa ni mwaka 2007, Dairekta na muigizaji wa filamu nchini, Single Mtambalike ‘Rich’ alimshawishi Rose Ndauka aingie kwenye tasnia ya sanaa.
Kama bahati, Rose alikuwa akienda kumtembelea rafiki yake katika Kundi la Kamanda ambalo Rich alikuwa akiigiza, ndipo akashawishiwa kujiunga na sanaa.
Rich, wasanii wenzake akiwemo Baba Haji, JB, alipomuona kwa mara ya kwanza aligundua kabisa kuwa Rose anaweza kuigiza ila alikuwa hajajitambui, hivyo baada ya kuoneshwa njia, fasta akaitumia fursa.
ALIPENDA KUTAZAMA FILAMU
Licha ya kutowahi kuigiza lakini Rose alipenda sana filamu za Kifilipino pamoja na tamthilia mbalimbali za Kizungu zilizokuwa zikiendelea kwenye runinga mbalimbali.
Risasi: Nje ya Rich kukuonesha njia, ujasiri zaidi wa kuendelea na uigizaji uliupata wapi?
Rose Ndauka: Baba Haji ndiyo alisisitiza kuwa naweza, alinipa ushawishi mkubwa, akaniambia nisikate tamaa, kweli nikajitahidi na mpaka leo hii napasua anga za uigizaji hadi kufikia hatua ya kupewa tuzo mbalimbali, namshukuru Mungu.
Risasi: Baada ya kuingia kwenye kundi la akina Rich, ilisemekana kuwa mlivuka mipaka na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na ndiyo maana ulikuwa na nafasi kubwa ya kucheza filamu, unalizungumziaje hilo?
Rose Nda
ka: Mh! Siwezi kusema kuwa ni kweli kwa sababu mimi ninachojua Rich alikuwa ni bosi wangu na mpaka leo namuheshimu kama bosi.
Rose Ndauka akiwa na mwanae
Risasi: Wakumbushe wasomaji wa Risasi Jumamosi filamu yako ya kwanza kabisa kuigiza.
Rose: Ilikuwa inaitwa Swahiba, nilicheza kama Aisha msichana aliyekuwa akisoma chuo.
Risasi: Tukitoka kwenye upande wa filamu na uigizaji, maisha ya kawaida kwako wewe kama msichana umewahi kuwa na uhusiano na wanaume tofauti na wengine waliripotiwa katika vyombo vya habari je, ni kwa nini uliamua kuwabwaga na kuhamia kwa baba mtoto wako (Maliki Bandawe) unaweza kusema?
Rose Ndauka: Niligundua kuwa hawakuwa na ‘future’ na mimi hivyo nikaachana nao, nikaamua kutulia na Maliki ambaye ndiye anayetarajia kunioa soon.
Risasi: Baba mtoto wako mlikutana wapi na una uhakika gani kama ana future na wewe?
Rose Ndauka: Mwanaume mwenye future utamjua tu, kwa huyu naamini nimefika, nilikutana naye Tanga tulikuwa tunafahamiana kabla ya kupendana na kilichotuweka karibu ni kazi hivyo, alivyorusha nanga nikaamua kumkubalia.
Risasi: Wewe ni staa unayependwa na wengi, unazungumziaje usumbufu kutoka kwa wanaume wakware? Baba mtoto wako anaipokeaje hali hiyo?
Rose: Niliwahi kusumbuliwa na wengi kabla sijaingia kwenye uhusiano kamili, kuna niliowahi kuwakubalia lakini kuna niliowakataa kwa sababu hawakuwa na vigezo, baada ya kuwa mama, najiheshimu na baba mtoto wangu ananiamini anachonikumbisha ni ‘ku-take care’ tu.
Risasi: Kuna habari zilitufikia wakati bado hamjapata mtoto na Maliki kuwa uliwahi kupigana klabu kwa kugombea penzi la njemba wa nje ya nchi, unalizungumziaje hili?
Rose: Mh! Siyo kweli, kwanza mimi starehe za klabu nilifanya sana nilipokuwa na umri wa miaka 19-21 baada ya hapo mtu akikwambia aliniona klabu atakuwa anakudanganya, sijakanyaga huko muda mrefu sana.
Risasi: Katika maisha yako umewahi kumfumania umpendaye?
Rose: Nimewahi kumfumania mpenzi (siyo Maliki) mara  mbili lakini nilichoshukuru ni kwamba sikuwahi kuachwa katika fumanizi, anayeachwa mara nyingi ni yule ninayemkuta na mpenzi wangu.
Risasi: Je, umewahi kumfumania baba mtoto wako? Ikitokea je utafanyaje?
Rose: Siombi itokee lakini ikishatokea ndiyo nitajua nifanyeje ila watu wasitegemee kama nikimfumania nitamuacha, nitafanya uchunguzi nitakapobaini sababu za kufanya hivyo, nitachukua uamuzi sahihi.
Risasi: Umewahi kupata skendo za kutembea na wapenzi wa rafiki zako akiwemo huyu baba mtoto wako, unalizungumziaje hilo?Rose: Sijawahi na hata baba mtoto wangu hajawahi kuwa na uhusiano na rafiki yangu yeyote kabla.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger