SHAMSA FORD: SINA SHOST BONGO MOVIES!

STAA wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford amefunguka kuwa hana rafiki yeyote maarufu ndani ya Bongo Movies.
Staa wa sinema za Kibongo, Shamsa Ford.

Akizungumza na paparazi wetu, Shamsa alisema kuwa tangu huko nyuma alishawafuta marafiki wote ambao ni wasaliti na badala yake mtu pekee ambaye ni rafiki yake ni mwigizaji mwenzake, Wellu Sengo ambaye anachipukia.

“Unajua ni bora uwe hata na rafiki mmoja ambaye anakujali na kukuthamini, wengine wote mimi niliwafutilia mbali kwa sababu ukiwa nao wengi wanaweza kukutia hata ‘stress’ zisizokuwa na maana kabisa,” alisema Shamsa

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger