WIKI iliyopita
katika makala haya tuliishia pale mwigizaji Wastara Juma alivyokimbizwa
na mumewe wa kwanza na kuokolewa na difenda la polisi, TUENDELEE…
APEWA TALAKA
Mwandishi: Nini kiliendelea baada ya purukushani hizo zote?
“Zilipita siku
tatu mume wangu alinipigia simu akiwa na dada yake na kunitamkia kwamba
ameniacha kwa talaka tatu na huyo dada yake ndiye shahidi na hiyo
ilikuwa mwaka 1999.
“Haikupita
miezi miwili alikuja nyumbani na kuandika talaka tatu za maandishi hivyo
nikawa nipo tu nyumbani na wakati misukosuko yote ikiendelea, mama
yangu alikuwa ameshafariki.
WASULUHISHWA
Mwandishi: Kwa hiyo katika kupewa talaka hizo hamkurudiana tena?
“Baada ya
kunipa talaka kwenye simu wazazi wake walikuja kusuluhisha tukarudiana
akaja kumchukua mtoto na akaenda kukaa naye Zanzibar huku mimi nikiwa
nimepata kazi ambapo mwanangu alikaa huko kwa mwaka mmoja nilipoenda
kumuona nikakuta ana utapia mlo ukweli nilisikia uchungu, niliwaambia
namchukua mwanangu akanipokonya na kwenda kujifungia naye chumbani
ambako nilienda na kuvunja mlango nikamchukua mtoto kwa nguvu ndipo
alipokaa kwa miezi miwili akaja kuniandikia talaka ya maandishi.
APATA MCHUMBA MWINGINE
Mwandishi: Je baada ya kupewa talaka ulipata mchumba mwingine?
“Ndiyo
nilipata mchumba ambaye kwa upande mwingine ni ndugu yetu ambaye alikuwa
anaishi hukohuko Zanzibar lakini nilishangaa siku moja nikiwa naye
pamoja na ndugu zangu wengine tumetoka kutembea, tulipofika nyumbani
polisi wakaingia na kutuulizia mimi na yule mchumba ambapo walituchukua
mpaka kituoni na nilipohoji walisema kwamba mume huyo wa zamani
amenifuma na mwanaume mwingine wakati yeye ndiye mume wangu.
Wastara Juma akipozi.
“Tulikaa selo
mpaka familia zote mbili zilipokuja na kuzungumza lakini hawakufikia
muafaka, nikaomba ile kesi ipelekwe mahakamani kwa sababu sikuwa mke wa
mtu, tukaenda mahakamani yule kijana ambaye ndiyo tulikuwa tunaanza
uchumba yeye hakuwa na makosa tukabaki mimi na huyo mwanaume.
“Ilikuwa ni
kama sinema kwani kila tulipokuwa tukikutana mahakamani tulikuwa
tunapigana sana mpaka mahakama ikaamua kutuhamishia kwenye mahakama ya
Kadhi (inayoshughulika na masuala ya ndoa) ambapo mwanaume huyo alidai
kwamba anataka arudishiwe mahari yake nikaomba kesi ihamishiwe Dar,
nikakubaliwa.
“Kabla
sijafika Dar nikakuta ameshaniwahi na kwenda BAKWATA ambako alitakiwa
anipe talaka lakini akaandika majina tu na kuondoka, Bakwata
walinisaidia tukapeleka mahakamani ambapo tangazo la mahakama kutoa
talaka lilitangazwa kwenye magazeti ya serikali kwa siku 39 ili mwenye
pingamizi apeleke lakini hakuna aliyejitokeza hivyo nikapewa talaka na
mahakama.
Mwandishi: Baada ya kumalizana na mumeo huyo uliendelea tena na yule mchumba?
“Niliendelea naye lakini tukiwa kwenye kuchunguzana siku moja nilikwenda kumtembelea kwao akaja mwanamke akawa anazungumza maneno mengi yakimhusu huyo mchumba kumbe alikuwa ni mwanamke wake, alipoondoka huyo jioni yake akaja mwingine akiwa anamuulizia na kesho yake akaja wa tatu ambaye alikuwa akilalamika kwamba huyo mwanaume anasikia ana mchumba wakati yeye ni mwanamke wake



No comments:
Post a Comment