Memba
wa Kundi la Tip Top Connection , Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ akipozi
kimahaba na mwanamuziki Mwanaisha Abdallah ‘Nyota Ndogo’.Ilidaiwa kwamba Tunda Man anapokwenda Kenya huwa anafikia nyumbani kwa Nyota Ndogo. “Wasanii wengi wanakuja Kenya wanajifanya kuja kufanya shoo kumbe wanawafuata wanawake zao ila mimi namsihi Tunda Man ajiangalie, yasije yakamkuta kama ya wasanii wengine walivyopewa masaa ishirini na nne wasikanyage Kenya tena,” kilisema chanzo hicho.
Baada
ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alimvutia waya Tunda
Man na kumpa hongera ya kummiliki Nyota Ndogo ambapo alikuja juu na
kudai kuwa anahisi anataka kuchafuliwa.“Kaka nadhani unajua kuwa nina mke na sijawahi kupata skendo kubwa kama hiyo, Nyota Ndogo namheshimu kama dada yangu na sijawahi hata kufikiria kumtongoza please achana na hiyo habari,” alijitetea Tunda Man bila kujua tuna picha zao za mahaba.


No comments:
Post a Comment