Showing posts with label TUNDAMAN. Show all posts
Showing posts with label TUNDAMAN. Show all posts

TUNDAMANI AFUNGUKA KUHUSU UVUMI KWAMBA ANAMFUKUZIA WEMA SEPETU

Na Ibrahim Mussa
MKALI wa kibao cha Msambinungwa, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’, amesema hana mpango wa kutoka kimapenzi na msanii wa filamu za maigizo, mwanadada Wema Sepetu kwa kuwa hawaendani kabisa.
Tunda Mana katika pozi na presenta wa Global TV Online, Pamela Daffa 'Pam D' wakati wa mahojiano hayo.
Akuzungumza na Global TV kupitia kipindi cha Mtu Kati, Tunda alisema kuwa hafikirii hata mara moja kama atakuja kutoka kimapenzi na staa huyo kwa kuwa watakuwa wanapishana kwenye baadhi ya mambo.
Tunda Man ndani ya studio za Global TV Online.
“Wema ni rafiki yangu kama walivyo marafiki wengine lakini kitu kikubwa sitamani kabisa aje kuwa mpenzi wangu kwa sababu tutakuwa tunapishana katika baadhi ya mambo na hizi ngumi ninazocheza nahisi nitampiga mpaka nitauwa,” alisema Tunda Man.
Read more >>

TUNDA MAN, NYOTA NDOGO WAKUTWA WAKICHEZEANA KIMAHABA, HII NI BAADA YA KULANA URODA!!!!!!!!

Memba wa Kundi la Tip Top Connection lenye maskani yake Manzese jijini Dar, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ na mwanamuziki wa nchini Kenya, Mwanaisha Abdallah ‘Nyota Ndogo’ wamenaswa laivu wakiwa kwenye pozi la mahaba niue.
Memba wa Kundi la Tip Top Connection , Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ akipozi kimahaba na mwanamuziki Mwanaisha Abdallah ‘Nyota Ndogo’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kutoka nchini humo, wawili hao walikuwa wakijiachia nyumbani kwa Nyota Ndogo huku kukiwa na madai mazito kuwa eti wanapika na kupakuwa. 
‘Tunda Man’ na ‘Nyota Ndogo’ wakila ujana.
Ilidaiwa kwamba Tunda Man anapokwenda Kenya huwa anafikia nyumbani kwa Nyota Ndogo. “Wasanii wengi wanakuja Kenya wanajifanya kuja kufanya shoo kumbe wanawafuata wanawake zao ila mimi namsihi Tunda Man ajiangalie, yasije yakamkuta kama ya wasanii wengine walivyopewa masaa ishirini na nne wasikanyage Kenya tena,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata maelezo hayo, kachero wa Ijumaa Wikienda alimvutia waya Tunda Man na kumpa hongera ya kummiliki Nyota Ndogo ambapo alikuja juu na kudai kuwa anahisi anataka kuchafuliwa.
“Kaka nadhani unajua kuwa nina mke na sijawahi kupata skendo kubwa kama hiyo, Nyota Ndogo namheshimu kama dada yangu na sijawahi hata kufikiria kumtongoza please achana na hiyo habari,” alijitetea Tunda Man bila kujua tuna picha zao za mahaba.
Read more >>

MSANII TUNDAMANI ATIWA MBARONI NA KUPIGWA PINGU

msanii wa bongo flava tundamani amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa kwa mda nchini Kenya kabla ya kuachiwa huru. tukio Zima lilitokea pale ambapo tundamani alshndwa kusimama kwenye kizuizi barabarani jambo lililowafanya maafisa wa polisi kumfukuza kwa nyuma na kumkamata wakijua ni gaidi. hata hvyo baada ya mahojiano ya mda mrefu tunda aliachiwa huru
Read more >>

TUNDA MAN AMTOLEA YA MOYONI EDWARD LOWASSA, SOMA ZAIDI HAPA

 
Kutana na ya moyoni mwa Tunda Man, staa wa bongofleva kutokea kundi la Tiptop Connection ambapo amepost picha kadhaa na maelezo yake kwenye mtandao wa instagram.
Ya kwanza ni hiyo hapo juu akiwa kasimama mbele ya mabango yanayomuhusu Mbunge wa Monduli Edward Lowassa anaetajwa sana kuhusu Urais wa Tanzania 2015 ambapo kwenye maelezo ya hiyo picha Tunda Man aliandika ‘fotmation yetu ni 4-4-2′

 
Post nyingine alizoweka Tunda man ni hizi hapa chini akiwa nchini Kenya ikiwa ni siku kadhaa tu baada ya kupona toka apate mshtuko na mwili kukosa nguvu sekunde chache baada ya kupokea simu ya namba asiyoifahamu ambayo sio ya Afrika Mashariki.
Read more >>

ILE NAMBA INAYOSEMEKANA NIYAFREMASON ILIYOMPIGIA TUNDA MAN YAPATIKANA, SIKILIZA MKASA MZIMA HAPA

2ndaa 
Hii stori ilianzia hapa hapa millardayoTV baada ya Tunda Man kusema kuwa amepigiwa simu na namba asiyoijua na kisha baada ya kuongea nae akaanza kuhisi hali ya utofauti katika mwili wake.
Soudy Brown kaenda mbali zaidi kwa kuipiga ile namba kisha kuwapigia mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA kwa ajili ya muongozo juu ya hiyo namba.
Read more >>

TUNDA MAN APIGIWA SIMU NA FREEMASON, AANGUKA NA KUZIMIA, SOMA ZAIDI MKASA HUU

Memba wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhan ’Tunda Man’ amekutwa na mauzauza baada ya kupokea simu yenye namba zinazodaiwa kuwa za ajabu na kumsababishia atokwe damu puani, mdomoni na kupooza upande mmoja.
Memba wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhan ’Tunda Man’ akiwa katika Hospitali ya Palestina.
Chanzo makini kilicho karibu na msanii huyo ambacho kilikuwa ndani ya Hospitali ya Palestina ambako Tunda Man alilazwa, kimeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea mwanzoni mwa wiki hii wakati staa huyo akifuturu.
“Alipigiwa na namba f’lani hivi ya ajabuajabu inayoishia na 39 kama mara 30 hivi, hakuipokea maana alishawahi kusikia juu ya namba za ajabu lakini baadaye akaamua kupokea ndipo ghafla akaanguka, akaanza kutokwa damu puani kisha kuzimia kabisa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Tulimfikisha Hosptali ya Palestina na hali yake ilikuwa mbaya sana lakini kwa jitihada za madaktari na manesi wamemsaidia kwa sasa kidogo anaendelea vizuri.”
Khalid Ramadhan ’Tunda Man’.
Baada ya kupata taarifa hiyo, Ijumaa lilimtafuta Tunda Man ili kutaka kujua undani wa sakata hilo, alipopatikana alifunguka:
“Nakumbuka nilipokea simu yenye namba nisizozifahamu ambayo iliita sana nikajishtukia kuipokea lakini baadaye nikahisi ni kama namba za nje ya nchi labda ni dili la kwenda kufanya shoo, nilivyopokea tu sikuwa nasikia mtu akiongea zaidi ya kusikia mtu kama vile anapuliza kitu.
“Baada ya hapo nikajiona naishiwa nguvu, damu zikinitoka puani na mdomoni kisha nikajikuta nipo Hospitali ya Palestina,” alisema Tunda Man.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger