Mwenyekiti
wa Serikali ya Kijiji cha Bago, Maulid Omary Tamla akionesha sehemu
alipofukiwa marehemu Asha Mrisho kwa mara ya kwanza .
Katika tukio hilo, mama huyo inadaiwa aliaga kuwa anakwenda Mbande,
Dar es Salaam kwenye harusi ya ndugu yake ambayo ilifanyika Juni mwaka
huu.Wifi wa Asha, Cheka Mrisho aliliambia gazeti hili kuwa marehemu
aliondoka nyumbani na hakuna aliyekuwa na wasiwasi kwa vile walielewa
alikuwa harusini.Aliongeza kuwa, baada ya kuona kimya, mtoto wake alipiga simu kwa ndugu zake wanaoishi Dar na kuulizia alipokuwa mama yake, alifahamishwa kwamba hakuonekana ndipo jitihada za kumtafuta zikaanza bila mafanikio.
Cheka alisema: “Kabla ya kuondoka Juni 26, mwaka huu, Asha alifanya mawasiliano na mtu ambaye simjui, hivyo nina wasiwasi huenda alitekwa.”Asha alipatikana Julai 28, mwaka huu baada ya siku 32 kupita akiwa amefariki dunia na kufukiwa katika shamba la mananasi la mtu aliyetajwa kwa jina la Abdallah Muligazi.
“Marehemu aligundulika na mbwa ambao walikuwa wakimnyofoa viungo vya mwili wake huku wakibweka na mfanyakazi wa shamba hilo aitwae Rashidi Ally alipokwenda kuangalia kuna nini, akaikuta maiti ikiwa imefukuliwa,” alisema Asha.
Ally alitoa taarifa kwa uongozi wa kijiji ambao uliita polisi na mwili ulipofukuliwa ulitambuliwa kuwa ni wa Asha, baada ya uchunguzi wa madaktari, wakaruhusu azikwe.Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bago, Maulid Omary Tamla aliliambia gazeti hili kuwa habari za marehemu kupotea zilifikishwa ofisini kwake siku ya kumi na tatu tangu aondoke nyumbani na kuongeza kuwa ndugu walisema aliaga anaenda harusini jijini Dar, ambapo alitafutwa bila mafanikio.
Ilibainika kuwa marehemu kabla ya kuondoka alibadilisha kadi ya simu aliyokuwa anaitumia na kuiacha chini ya mto nyumbani kwake ambayo iligunduliwa na polisi wakati wa upekuzi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, SACP Ulrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Mpaka sasa tunawashikilia watu wawili ambao siyo wenyeji wa kijiji hicho kwa uchunguzi,” alisema Kamanda Matei.
No comments:
Post a Comment