Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwimbaji
ambaye ni Prezidaa wa Bendi ya Mikumi Sound, Joshua Malekela
amelazimika kumtimua mwanamke mmoja ukumbini, kisa kikielezwa ni
mcharuko.
Tukio hilo la aina yake lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Ukumbi wa
Black Poiny uliopo maeneo ya Iringa Road, Msamvu mjini hapa ambapo bendi
hiyo ilikuwa ikishusha burudani.
Kabla ya kutimuliwa, mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana, alikuwa akicheza ovyo na kuparamia waume za watu.
Pia kabla ya kutolewa, mwanamke huyo alionekana akikwidwa na shabiki
wa bendi hiyo akimshutumu kujipendekeza kwa mumewe kwa kumlazimisha
akacheze naye sebene huku akimwaga ‘lazi’ hadharani.
Baada ya uongozi wa bendi kulalamikiwa juu ya mwanamke huyo, ndipo
prezidaa huyo akaita mabaunsa na maafande wa ukumbi huo na kuwaamuru
kumtoa nje mara moja, jambo ambalo lilitekelezwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment