Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’akiwa na mrembo huyo.
Ishu hiyo ilijiri Jumamosi ya Septemba 20, 2014 ndani ya Uwanja wa
Jamhuri mjini hapa wakati wa pambano kati ya Yanga na Mtibwa Sugar
katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo wenyeji walishinda 2-0. Steve
alitinga uwanjani saa 11:00 jioni akiwa na demu huyo mrefu
kwake,aliyetinga kipensi cha jinzi kifupi na tisheti ya njano na kijani
(zinazotumiwa na Yanga).
Wakati wawili hao wakipita kwenye jukwaa la mashabiki wa Simba, ndipo
walipozomewa na wengine kuwarushia chupa za maji kwa kile kilichodaiwa
kuwa, demu huyo alivunja maadili ya Kitanzania kwa kuvaa kihasara
hadharani.
Mrembo huyo akikatiza mbembezoni mwa uwanja.
Baadaye mwandishi wetu alimfuta Steve na kuzungumza naye kuhusu tukio
hilo ambapo alisema: “Wale kunizomea ni haki yao ila mimi na mwenzangu
tumeona kama wametushangilia.”
Alipoulizwa uhusiano wake na demu huyo,Steve aligoma kujibu badala yake
alikimbilia kwa mwandishi mwingine wa Global Publishers (Musa Mateja) na
kuomba msaada. Mrembo huyo alipotakiwa kuzungumzia tukio hilola
kuzomewa na sababu za yeye kuvaa vile, alijibu kwa mkato: “Kuzomea ni
haki yao, mimi nawaona kama washamba tu.”

No comments:
Post a Comment