UNAENDELEA na makala haya tuliyoyaanza wiki iliyopita, mwigizaji Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka vitu vingi vinavyohusu maisha yake.
ENDELEA…
Mwandishi: Ulijisikiaje siku ambayo Mike alienda kujitambulisha kwenu rasmi?
Thea: Kwanza sikuwa naamini kama ni kweli bali niliamini siku hiyo
ambayo Mike alipeleka mahari nyumbani, yaani hata hatukuwa tumekuwa na
uhusiano wa kimapenzi, ilikuwa kama utani. Baada ya kupeleka mahari na
utaratibu wa kufunga ndoa kuanza ndipo tulipoonjana.
Mwandishi: Mlifunga ndoa mwaka gani, na mlikaa kwenye uchumba kwa muda gani?
Thea: Tulifunga ndoa mwaka 2010 na kwenye uchumba hatukukaa kwa muda mrefu ni kama miezi sita tu.
Mwandishi: Unayazungumziaje maisha ya ndoa?
Thea: Maisha ya ndoa ni mazuri lakini yana changamoto zake kwa sababu hapa duniani kila kitu kina changamoto zake.
Mwandishi: Kuna kipindi mlitengana na mume wako nini sababu?
Thea: Ni kweli mwaka 2013 mwishoni tulitengana sababu siwezi kuziweka
wazi kwani ni mambo ya siri zaidi na siyo maadili kuanika mambo ya ndoa
kwenye kadamnasi lakini nashukuru mwaka huu tumerudiana na hii ni baada
ya kukaa wawili na kukubaliana huku tukimaliza tofauti zetu.
Mwandishi: Vipi ndoa yako kwa sasa inaendeleaje?
Thea: Namshukuru Mungu ndoa yangu ina amani na tuna furaha tele.
Mwandishi: Mpaka unaingia kwenye ndoa uliwahi kutoka na wanaume wangapi ambao ni wasanii wenzako?
Thea: Katika maisha yangu sijawahi kutoka kimapenzi na msanii
mwenzangu tangu niingie kwenye hii sanaa ya filamu mpaka nilivyokutana
na Mike Sangu.
Mwandishi: Ni kitu gani kibaya kiliwahi kukutokea na hutakisahau?
Thea: Katika maisha yangu kitu ambacho kilinitokea kibaya na
sitakisahau ni wakati nilipotengana na mume wangu Mike watu waliongea
maneno mengi sana ya kuumiza ila nikawa namuomba Mungu tu maana neno
linasema; “Usifurahie mtu akianguka.” Siku moja atasimama tena na
ukimuona mtu ameacha ndoa huwezi kujua kilichomtoa ni nini.
Mwandishi: Ni kitu gani ambacho unakipenda sana?
Thea: Ninapenda
vitu vingi lakini cha kwanza nampenda sana Mungu nimeokoka na sijawahi
kwenda kwa mganga tangu nizaliwe wa pili ni mume wangu ndiyo wengine
wanafuata.
Mwandishi: Kitu gani kizuri ambacho hutakisahau maishani mwako?
Thea: Kitu kizuri ambacho huwa sisahau na sitosahau ni siku
niliyojifungua mwanangu wa kwanza yaani nilifurahi sana kwani nilikuwa
mtoto bado hata siku uchungu unaniuma sikujua ila nilikuwa nasikia
maumivu makali mno.
Mwandishi: Kuna tetesi kwamba wasanii huwa mnalogana sana, kwako hili likoje?
Thea: Mimi siamini kama kuna uchawi kwenye tasnia na sijawahi kufanya
mambo hayo na katika maisha yangu hakuna anayeweza kuniloga kwa sababu
nina Yesu ndani yangu.
Mwandishi: Unazungumziaje watabiri waliotabiri vifo vyenu wasanii?
Thea: Nasema kwamba watabiri wote waliotabiri kwamba sisi wasanii
tutakufa ni maajenti wa shetani kwa sababu kwa nini hawajatoa utabiri
mtimilifu kwani hatujaambiwa labda tuache maovu, kwani kuacha dhambi
siyo kitu rahisi tunatakiwa sisi wasanii tuombewe na tuombe pia neema ya
Mungu ituokoe.
Mwisho!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment