Showing posts with label THEA. Show all posts
Showing posts with label THEA. Show all posts

THEA: MIKE ALIONA NDANI BAADA YA KUNILIPIA MAHARI, SONGA NAYO HAPA

UNAENDELEA na makala haya tuliyoyaanza wiki iliyopita, mwigizaji Salome Urassa ‘Thea’ amefunguka vitu vingi vinavyohusu maisha yake.
ENDELEA…

Salome Urassa ‘Thea’
Mwandishi: Ulijisikiaje siku ambayo Mike alienda kujitambulisha kwenu rasmi?
Thea: Kwanza sikuwa naamini kama ni kweli bali niliamini siku hiyo ambayo Mike alipeleka mahari nyumbani, yaani hata hatukuwa tumekuwa na uhusiano wa kimapenzi, ilikuwa kama utani. Baada ya kupeleka mahari na utaratibu wa kufunga ndoa kuanza ndipo tulipoonjana.

Mwandishi: Mlifunga ndoa mwaka gani, na mlikaa kwenye uchumba kwa muda gani?
Thea: Tulifunga ndoa mwaka 2010 na kwenye uchumba hatukukaa kwa muda mrefu ni kama miezi sita tu.

Mwandishi: Unayazungumziaje maisha ya ndoa?
Thea: Maisha ya ndoa ni mazuri lakini yana changamoto zake kwa sababu hapa duniani kila kitu kina changamoto zake.

Mwandishi: Kuna kipindi mlitengana na mume wako nini sababu?
Thea: Ni kweli mwaka 2013 mwishoni tulitengana sababu siwezi kuziweka wazi kwani ni mambo ya siri zaidi na siyo maadili kuanika mambo ya ndoa kwenye kadamnasi lakini nashukuru mwaka huu tumerudiana na hii ni baada ya kukaa wawili na kukubaliana huku tukimaliza tofauti zetu.
Mwandishi: Vipi ndoa yako kwa sasa inaendeleaje?

Thea: Namshukuru Mungu ndoa yangu ina amani na tuna furaha tele. 
Mwandishi: Mpaka unaingia kwenye ndoa uliwahi kutoka na wanaume wangapi ambao ni wasanii wenzako?


Thea: Katika maisha yangu sijawahi kutoka kimapenzi na msanii mwenzangu tangu niingie kwenye hii sanaa ya filamu mpaka nilivyokutana na Mike Sangu.

Mwandishi: Ni kitu gani kibaya kiliwahi kukutokea na hutakisahau?
Thea: Katika maisha yangu kitu ambacho kilinitokea kibaya na sitakisahau ni wakati nilipotengana na mume wangu Mike watu waliongea maneno mengi sana ya kuumiza ila nikawa namuomba Mungu tu maana neno linasema; “Usifurahie mtu akianguka.” Siku moja atasimama tena na ukimuona mtu ameacha ndoa huwezi kujua kilichomtoa ni nini.

Mwandishi: Ni kitu gani ambacho unakipenda sana?
Thea: Ninapenda vitu vingi lakini cha kwanza nampenda sana Mungu nimeokoka  na sijawahi kwenda kwa mganga tangu nizaliwe wa pili ni mume wangu ndiyo wengine wanafuata.
Mwandishi: Kitu gani kizuri ambacho hutakisahau maishani mwako?
Thea: Kitu kizuri ambacho huwa sisahau na sitosahau ni siku niliyojifungua mwanangu wa kwanza yaani nilifurahi sana kwani nilikuwa mtoto bado hata siku uchungu unaniuma sikujua ila nilikuwa nasikia maumivu makali mno.

Mwandishi: Kuna tetesi kwamba wasanii huwa mnalogana sana, kwako hili likoje?
Thea: Mimi siamini kama kuna uchawi kwenye tasnia na sijawahi kufanya mambo hayo na katika maisha yangu hakuna anayeweza kuniloga kwa sababu nina Yesu ndani yangu.
Mwandishi: Unazungumziaje watabiri waliotabiri vifo vyenu wasanii?

Thea: Nasema kwamba watabiri wote waliotabiri kwamba sisi wasanii tutakufa ni maajenti wa shetani kwa sababu kwa nini hawajatoa utabiri mtimilifu kwani hatujaambiwa labda tuache maovu, kwani kuacha dhambi siyo kitu rahisi tunatakiwa sisi wasanii tuombewe na tuombe pia neema ya Mungu ituokoe.
Mwisho!
Read more >>

HIKI NDIO USICHOKIJUA KUHUSU THEA

Mpenzi msomaji wa safu hii ya Exclussive Interview baada ya kumaliza kusoma historia ya maisha ya msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma, leo tunakuletea msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.Thea amefunguka mengi kuhusiana na maisha yake ya sanaa, karibu uinjoi mahojiano:
Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salome Urassa ‘Thea’.
HISTORIA KWA UFUPI
Nimezaliwa mwaka 1982 mkoani Shinyanga, nimepata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Igunda iliyopo Kahama ambapo nilisoma mpaka darasa la tatu na baada ya hapo nilihamia Shule ya Msingi Mapambano-Sinza, jijini Dar na kufanikiwa kuhitimu darasa la saba.

SEKONDARI            
Baada ya kuhitimu nilijiunga na kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Zanaki ambako nilisoma kwa mwaka mmoja tu na kuhamia Sekondari ya Gorio ambako nako nilisoma kwa mwaka mmoja nikahamia Kijitonyama ambako nilimalizia kidato cha tatu na cha nne.

APATA UJAUZITO
Baada ya kuhitimu kidato cha nne niliendelea kusoma masomo ya Pre Form Five lakini ndoto zangu zilikwamia hapo baada ya kupata ujauzito.

BAHATI MBAYA
Ilitokea bahati mbaya tu na sikuona sababu ya kutoa mimba ndiyo nikaamua kuzaa na nikapata mtoto wa kiume ambaye kwa sasa baba yake alimchukua anasoma Dubai.

Mimba hiyo niliipata mwaka 2003 nikiwa najiandaa na masomo ya kuingia kidato cha tano, nilipata ujauzito na kuamua kuzaa ambapo nilipata mtoto wa kiume anayejulikana kwa jina la Maron Bimpela.
HAWAKUWA NA MALENGO YA NDOA
Sisi hatukuwa na malengo ya kuoana bali nilipopata ujauzito na kujifungua baba mtoto aliendelea kumtunza mtoto mpaka alipokuwa mkubwa akaja kumchukua, ndoto zangu za kusoma ziliishia hapo.

RASMI KWENYE SANAA
Baada ya kujifungua sikuendelea tena na masomo bali niliendelea na sanaa kwani tangu nikiwa kidato cha nne nilikuwa nafanya sanaa hivyo niliingia rasmi.

AKUTANA NA CHIKI
Kwa mara ya kwanza kabisa Chiki Mchoma ndiye aliyenichukua akanipeleka kwenye kundi lililokuwa linajulikana kwa jina la Tunda.

MCHEZO WAKE WA KWANZA
Mchezo wa kwanza kushiriki na kurushwa Runingani uliitwa Ulimwengu wa Vijana ukweli siku hiyo sikulala kutokana na furaha niliyokuwa nayo. Kwenye kundi hilo nilidumu kwa muda mfupi sana, kama miezi tu.

AJIUNGA NA MAMBO HAYO
Baada ya hapo nilijiunga na Kundi la Mambo Hayo baadaye Kaole na hapo mpaka sasa naendelea kucheza filamu ambapo nina filamu za kwangu mwenyewe sita na nyingine zaidi ya 40 za kushirikishwa.

UHUSIANO NA BABA MTOTO
Baada ya kujifungua sikuendelea na uhusiano na baba mtoto wangu. Uhusiano uliokuwepo ni kwamba alikuwa akimlea mwanaye tu na baada ya kukua ndipo akamchukua.

AACHANA NA WANAUME
Baada ya kupata mtoto wangu nilitulia na kumlea na sikuwahi kujihusisha kimapenzi na mwanaume yeyote.Nilikaa miaka mingi sana mpaka nilipokuja kukutana na Michael Sangu ‘Mike’, tukafunga ndoa.

WALIVYOKUTANA
Mimi na Mike tulikuwa kwenye kundi moja ambapo nilikuwa namuita kaka na yeye ananiita mdogo wake lakini alikuwaga ananitania kwamba lazima atanioa nikawa naitikia kiutani tu.

Yaani sikuwa hata na wazo la kuolewa na msanii na nilikuwa nimeshaapa kwamba sitaolewa na msanii sijui ni kitu gani kilitokea maana Mike nilikuwa nimemzoea namuita kaka tukawa tunapiga stori sana lakini kila wakati alikuwa akiniambia atanioa nikawa namjibu sawa.
Read more >>

THEA AFUNGUKA MANENO MAZITO KUHUSU MASUALA YA KIMAPENZI NA KUSEMA " NDOA SIYO PETE", SOMA KWA UNDANI ZAIDI

Msanii wa muda mrefu katika filamu Bongo, Salome Urassa maarufu kama Thea,  amejinasibu kuwa kutovaa kwake pete ya ndoa haimaanishi chochote kwa vile kitu hicho siyo muhimu.
Msanii wa muda mrefu katika filamu Bongo, Salome Urassa maarufu kama Thea wakati wa kufunga ndoa.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati, Thea alisema awali alikuwa akivaa pete, lakini bahati mbaya ilipotea na kupotea huko hakumaanishi kwamba ndoa yake imepotea.
“Sitaki kuamini kabisa kama ndoa ni pete, ninachojua ni kwamba siku zote ipo moyoni, unaweza kuvaa hata pete kumi kidoleni, lakini kama haina amani ni kazi bure tu, mimi sina lakini kama nina furaha kwenye ndoa yangu hakuna neno,” alisema.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger