
Ndiyo
maana ukiwa hauko sawa kimapenzi, namaanisha ukiwa huna mpenzi wakati
unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha, hata mambo mengine
huwezi kuyafanya kwa ufasaha.
Lakini
yule ambaye maisha yake ya kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka
kutoka kwa mpenzi wake, utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na
furaha haikauki.Wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila
siku kwa sababu ya kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao. Kuna
ambao kusalitiwa kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa sababu hawajui
yapi wayafanye ili wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao.
Kimsingi
nimegundua wengi hatuna elimu ya kutosha juu ya mapenzi. Unakuta mtu
kaanzisha uhusiano na mtu ambaye yuko mbali lakini hajui wanawezaje
kulidumisha penzi lao. Mmeoana wote mnafanya kazi na ni wanandoa,
mnawezaje kuishi katika msingi sahihi? Hayo yote utayajua endapo tu
utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu kuhusu mambo
hayo.
Huenda
wewe tangu umezaliwa hujawahi kujihusisha kimapenzi, leo umeingia
kwenye uhusiano na hujui chochote, kama huna elimu ya mapenzi hata kama
umzuri vipi, utaachika tu kama siyo kusalitiwa kila siku.
Ndiyo
maana leo nimeleta mada hii ili kama ulikuwa hujui, uanze leo
kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba. Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi
ya kiutu uzima, yale ambayo huwezi kufundishwa shuleni, kusoma kwenye
magazeti, kuona kwenye vipindi vya kawaida vya televisheni au
kusikisiliza redioni.

Mtandaoni
Mitandao
imekuwa ni msaada sana katika ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo
utalihitaji usilipate kwenye mtandao. Kwa maana hiyo basi, kama kuna
jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi, kuwa rafiki wa mitandao husika.
Kwa
mfano unataka kujua jinsi unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako mkiwa
faragha. Ukiuliza mtandao, utakuletea.Licha ya kwamba lugha unayotumika
ni ya Kiingereza, naamini wengi wetu tunajua hata kama ni cha
kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada ukiandika kwa Kiswahili pia unaweza kuzipata.
Majarida maalum
Yapo
majarida yanayozungumzia mapenzi kwa undani wake ambayo yanauzwa sehemu
maalum kwa jili ya watu wazima tu. Kama kweli wewe ni mtu mwenye
uhitaji wa majarida hayo, ukiulizia utayapata kwani huwezi kuyakuta
yanauzwa kiholela.
Wakati
mwingine yanauzwa bei kubwa lakini elimu utakayoipata ni kubwa na
huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la
shilingi 50,000 na ndani yake ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na
mpenzi wako, namna na kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi
wako muwapo faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo
ukilinganisha na gharama ulizotumia kwenye harusi yenu?
Ongea na wataalam
Kuna
wataalam wa mambo ya mapenzi ambao wanaweza kukusaidia. Kwa mfano mimi
nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi kushauri wasomaji wangu juu ya
mambo yanayowakosesha furaha katika maisha yao ya kimapenzi.
Siyo
mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi ya akina mama ambao wamekuwa
wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana kabla ya kuingia kwenye
ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza
mambo sahihi kuhusiana na mapenzi. Nilichogundua mimi ni baadhi ya watu
kuwa na aibu. Hivi unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo
unajua kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?
Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa
watu wenye uchu na elimu hasa hii nyeti, inabidi wakati mwingine
wakubali kuamka usiku na kuangalia vipindi ambavyo vinazungumzia mapenzi
kwa watu wazima.Mara nyingi vipindi hivi huwezi kuviona mchana,
wanaovirusha husubiri muda ambao watoto wamelala. Ukiwa ni mpenzi wa
kuvifuatilia vipindi hivi, ni lazima utakuwa bora kwenye uhusiano wako.
Nunua CD
Huenda
hata wewe una CD zako ambazo mara nyingi unaziangalia usiku kabisa,
ukiwa peke yako au na mwenza wako. Hilo ni jambo zuri hasa linapokuja
suala la kujiweka fiti kimapenzi.
Katika
hili naomba niseme tu kwamba, kuna ambao wanazitumia CD hizi
kujiharibu. Wanazinunua ili kujifunza mambo kadhaa lakini mwisho wake
wananogewa na kujikuta wakimaliza haja zao kwa kuziangalia.
Niwaonye
tu kwamba, ukizoea sana kuziangalia picha hizo ukiwa peke yako kisha
ukamaliza shida zako, unaweza kujikuta si mtu unayependa kuwa na mpenzi
tena. Wapo ambao leo hii hawataki kusikia kitu mpenzi, kisa
wakiangalia CD hizo humaliza haja zao! Ni sawa unaweza kumaliza haja
zako lakini madhara yake ni makubwa. Ndiyo maana nasema kwamba, tumia CD
hizo kujipatia ujuzi lakini si kumalizia haja zako.
Ni
hayo tu ila kama unataka kujifunza zaidi kupitia mimi, usisite
kunitafuta. Kumbuka ujanja na ubunifu wako ndivyo vinaweza kudumisha
ndoa yako lakini ukiwa unaendesha maisha yako kibubusa, kaa mkao wa
kusalitiwa kama siyo kuachwa!
No comments:
Post a Comment