Showing posts with label AMANDA. Show all posts
Showing posts with label AMANDA. Show all posts

AMANDA AZUA TIMBWILI MTAANI

Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ hivi karibuni alizua balaa la aina yake baada ya kukatiza mtaani akiwa amevaa kigauni kilichokaribia kuacha wazi makalio yake.
Msanii wa filamu, Tamrina Posh ‘Amanda’ akiwacharukia wanaume waliokuwa wanampigia miluzi huku wakimzodoa.
Tukio hilo lililowashangaza wengi lilijiri eneo la Mwenge Bamaga jijini Dar wakati msanii huyo alipokuwa akitembea kuelekea kwenye mgahawa uliopo eneo hilo.
Huku akitembea kwa staili ya ‘hamsini…mia…hamsini…mia…’, Amanda alionekana kufanya makusudi kwani kadiri wanaume walivyokuwa wakijikusanya kumshangaa, ndivyo alivyoongeza mikogo na kuwaacha miudenda ikiwatoka.
‘Amanda’ akiingia kwenye gari kuondoka 
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wanaume ambao wengi wao ni madereva wa Bajaj na mafundi gereji walionekana kumzodoa huku wakieleza kuwa, ni msanii asiyejiheshimu.
“Yule kutuvalia sisi vile ndiyo nini? Mavazi yale yanavaliwa klabu usiku tena wanaovaa vile ni wale wasioithamini miili yao, tukisema anatutangazia biashara tutakuwa tunakosea?” alihoji fundi mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma.
Tamrina Posh ‘Amanda’ akipozi.
Katika kujua sababu ya kuvaa kigauni hicho, mwandishi wetu alimfuata Amanda lakini kabla ya kuulizwa chochote aliingia kwenye gari na kuondoka zake baada ya kuwachimba mkwara waliokuwa wakimpigia miluzi. Baadaye alipopigiwa, simu iliita bila kupokelewa
Read more >>

HIZI NDIO SABABU ZA AMANDA KUTOKUZAA

STAA wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ amefunguka kuwa mpaka sasa hajazaa kwa sababu bado alikuwa hajamuona mwanaume wa kuwa baba watoto wake.
Staa wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’
Akichonga na gazeti hili, Amanda alisema katika maisha yake anapenda sana mtoto lakini bado hajatokea mwanaume sahihi wa kuzaa naye ila anashukuru kwa sasa amempata.
“Miaka yote sijazaa kwa sababu nilikuwa sijamuona mwanaume sahihi wa kuzaa naye, lakini kwa sasa nimemuona japokuwa siwezi kumtaja kwa sababu bado naye nipo katika hatua za mwisho za kumpitisha kama anafaa,” alisema Amanda.
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger