Showing posts with label BBA. Show all posts
Showing posts with label BBA. Show all posts

UNDANI NA PICHA ZAIDI JUU YA KUUNGUA KWA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA, SOMA ZAIDI HAPA

JUMBA lililokuwa limeandaliwa kwa ajili ya
washiriki wa shindano la Big Brother Africa
(BBA ) 2014 limeteketea kwa moto jana eneo la
Sesani Studios jijini Johannesburg nchini
Afrika Kusini.
Kuteketea kwa jumba hilo kumesababisha
uzinduzi wa shindano hilo kwa mwaka huu
kusogezwa mbele tofauti na awali ambapo
ulitarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya
Septemba 7, mwaka huu .
Katika taarifa iliyotolewa na waandaaji wa
shindano hilo, M- Net na Endemol ni kwamba
katika ajali hiyo hakuna aliyejeruhiwa na
chanzo cha moto huo bado hakijafahamika
huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo
chake.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa kwa sasa
linatafutwa jumba lingine litakapoendeshwa
shindano hilo linalochukua siku 91 .
Read more >>

ZAWADI YA MSHINDI WA BIG BROTHER MWAKA HUU, RATIBA NA KILA KITU VYATAJWA



Shindano la Big Brother Africa 2014 limetangaza tarehe za usaili katika nchi mbalimbali za Afrika zitakazoshiriki huku kwa Tanzania tarehe ya usaili ikipangwa kuwa 11-12 July katika hoteli ya New Africa Hotel, Dar es salaam. 


Mshindi wa mwaka huu atajinyakulia kitita cha $300,000.

Nchi zinazoshiriki mwaka huu ni Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger