Showing posts with label MADEE. Show all posts
Showing posts with label MADEE. Show all posts

ANGALIA MADEE ALIVYOSOTESHWA POLISI

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ hivi karibuni alilala katika Kituo cha Polisi cha Kigamboni, Dar  akihusishwa na utekaji wa dereva wa bodaboda, Suedi Waziri (pichani) kisha kumpa kipigo ambapo inadaiwa alisoteshwa kinomanoma.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva a.k.a Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’ akiwa mikononi mwa Polisi.
Baada ya tukio hilo lililotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, Ijumaa lilinasa picha zinazomuonyesha msanii huyo akihenyeshwa kituoni hapo huku mmoja wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo akinyetisha kuwa, licha ya ustaa wake Madee alikiona cha mtemakuni.
Dereva wa bodaboda, Suedi Waziri aliyetekwa na kushambuliwa na Madee.
“Mimi nilikuwepo pale kituoni, nilimshuhudia akiwa amepigwa pingu huku polisi kama sita hivi, mmoja akiwa na silaha wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi wakimpeleka mahakamani.“Alionekana aliyechoka sana huku akiwa na hofu ila inavyodaiwa baadhi ya watu wake wa karibu walikuwa wakihaha kumnusuru baada ya kulala selo,”  kilidai chanzo hicho.
Majeraha ya mguuni aliyopata Suedi Waziri baada ya kushambuliwa na Madee.
Kufuatia msala huo, msanii huyo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kigamboni na baadaye kuwekewa dhamana na baba yake ambapo kesi yake itatajwa tena Oktoba 6, mwaka huu.
Madee anadaiwa kumteka Suedi na kwenda kumsulubu nyumbani kwake Manzese baada ya kijana aliyekuwa amepakia kwenye bodaboda yake kukwapua simu ya msanii huyo na kukimbia.
Katika kushinikiza simu yake irudishwe ndipo Madee alipomtaiti Suedi na mwisho wa siku akaishia mikononi mwa polisi kwa kufunguliwa kesi iliyosomeka: VJB/RB/625/2014 KUTEKWA KWA BINADAMU
Read more >>

SAKATA LA MSANII MADEE KUTIWA NGUVUNI KWA KOSA LA UKABAJI , HII HAPA PICHA KAMILI

Taarifa zimethibitishwa kuhusu msanii kutoka kundi la TipTop Connection kushikiliwa na Polisi. 
Kabla ya kuongea na meneja wa kundi hilo ambae ni Babtale, Gossip Cop Soudy Brown kwenye You heard  alisema ‘inasemekana Jumamosi iliyopita Madee aliporwa simu yake na watu wawili usiku huko Kigamboni’Babtale alipoulizwa akasema ‘Kwenye mida ya saa tisa usiku Madee wakati anatoka kwenye show Kigamboni kuna waporaji simu wakiwa kwenye pikipiki wakampora kwa hiyo ikabidi gari aliyokuwemo Madee ikiendeshwa na Kwebe ianze kuikimbiza ile pikipiki alafu wakaigonga pikipiki kwa nyuma, pikipiki ilivyodondoka yule aliekua nyuma kwenye pikipiki ambae ndio alipora simu akafanikiwa kukimbia hivyo wakaishia tu kumkamata aliekua anaendesha hiyo pikipiki’ 

‘Wakamchukua na kwenda nae maskani Tiptop… mama yake akaja akasema msipeleke Polisi mwekeni hapa mi nakwenda kuwachukulia vitu vyenu, Madee kwa sababu alikua anakwenda kwenye show Mwanza ikabidi aende zake…… saa nne asubuhi yule mama akaja na Polisi badala ya kuja na mwizi mwenzake akaja na Polisi kataka kuwaokota watoto wote ofisini kwangu pale Tiptop, walimchukua huyo Muhalifu kwenye Land rover mpaka Polisi Magomeni na kubadilisha kibao kwamba huyu mtuhumiwa alitekwa’
Read more >>

BAADA YA KUKAA KWA MUDA MREFU SASA MADEE AFUNGUKA KUHUSU KUOA

Hamadi Ally aka Raisi wa Manzese aka Madee
anayetamba na wimbo wake ”Ni shidaa” ikiwa pia
ndiyo msemo wa Fiesta 20014, azungumzia
mahusiano yake ikiwa umri unakwenda na
hajaweka wazi tangu kufariki mpezi wake Tunda
miaka kadhaa iliyopita.
”Ni shidaa kwa sasa ndiyo habari ya mjini kiukweli,
wakati nabadilika watu wengi walisema nitabuma
lakini nashukuru Mungu sana haijakuwa hivyo na
kwa sasa kati ya wasanii ambao wanapiga show
nyingi kwa mwaka mimi mmoja wapo.Pia
kubadilika kwangu kumenifanya niwe na mafanikio
kuliko miaka mingi nilipokuwa nafanya mziki wa
silias Hip Hop nimejifunza kudhubuti bila ya
kumuangalia yeyote yule.Ni kweli tangu kufariki
kwa mpenzi wangu Tunda sijaweka wazi
mahusiano yangu siyo kwamba sipo kwenye
mahusiano hapana, ila itakapofikia wakati kila kitu
kitakuwa wazi siyo kila kitu kiwe open kwa sasa
nimekuwa so nafanya mambo huku nikiwa najua
nina mtoto na nahitaji ajifunze vitu vizuri kutoka
kwangu.Kuoa kwa sasa bado kuna malengo yangu
bado hayajitimia unajua unapomchukua mtoto wa
watu kuna mambo mengi sana na ndoa siyo kitu
cha mchezo so bado nipo nipo sana.”
Read more >>
 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger