ALIYEJIITA “MHUBIRI” AKAMATWA KWA UTAPELI WA KUDAI MALIPO KABLA YA HUDUMA.


Picture
Mtuhumiwa Richard Mwangusi
Jeshi la  polisi mkoa wa Iringa limemkamata na kumtupa mahabusu mhubiri  Richard Mwangusi, raia wa nchini uganda kwa  tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii baadhi ya watu wameeleza kusikitishwa na  kito cha utapeli kinachofanywa na  mhubiri huyo ambaye  amekuwa akiishi katika nyumba ya kulala  wageni ya Wihanzi mjini  Iringa kuwa amekuwa akiwataka  watu kutuma pesa kwa  njia ya  M-PESA kuanzia TSh 10,000 na kuendelea iwapo wanahitaji kupanga muda wa kuongea na mhubiri  huyo kupitia simu ya kiganjani.

Baadhi ya  wananchi  ambao  walitoa malalamiko yao leo  walidai kuwa  mhubiri  huyo amekuwa akitumia namba ya simu ya Lodge ya Wihanzi ambayo ni 0262700222 kwa kuwataka   watu  wenye matatizo  kupiga simu kwa namba hiyo na mara  baada ya  kupiga simu mhudumu  ambaye  yupo  zamu amekuwa akimtaka  mtu aliyepiga   simu  kueleza shida yake na mara  baada ya kueleza iwapo anataka kuongea na mhubiri  huyo amekuwa akitaka kutumiwa kwanza kiasi cha fedha kwa namba ya mhubiri huyo ndipo apewe huduma anayotaka.

Mmoja kati ya watu ambao  wamepata  kulizwa na mhubiri huyo amedokeza  kuwa namba  za mhubiri  huyo amezipata  kupitia kituo kimoja  cha  Radio  mjini Iringa  na kutokana na baadhi ya watu kutoa ushuhuda  kuwa  wamepona magonjwa sugu  ndio sababu ya kuchukua namba yake  ili  kuweza  kuombewa  pia ila baada ya kuchukua namba  hiyo amejikuta akiishia  kuliwa  pesa bila kupewa huduma husika.

Pia  alisema  kila anapomtafuta mhubiri huyo kwa njia ya simu  ili kuombewa amekuwa akimtaka  kuongeza pesa zaidi  ili  kuombewa hadi kupona jambo ambalo amekuwa akijiuliza kama kwa sasa injili ya biashara na kama  biashara  basi  ni  vyema wahubiri watangaze  bei  kamili  ili mtu anunue kulingana na uwezo wake.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger