BOMOA BOMOA YA POMBE MAGUFULI YAANZA.....JENGO LA BUSINESS PARK ( GREEN ACRES ) LABOMOLEWA

 a
 Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua, hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya wale walioonekana kukaidi agizo hilo. 


Katika kutekeleza agizo hilo zoezi hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande hizo chini ya usimamizi ya Askari
 Msongamano pande hizo.....
 Tayari ukuta ukiwa umeshashushwa chini wa upande wa barabarani  huku baadhi ya watu wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakihaha kuhamisha baadhi ya vifaa.
 Wakati likianza zoezi hilo ndani walikuwapo watu wanaoendesha shughuli zao katika jengo hilo.
 Baadhi ya wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakiduaa wasijue la kufanya.......
 Umeshashushwa upande mmoja.
 Huu ni upande wapili wa jengo hilo.
 Ni upande wa mbele wa jengo hilo zima unavyoonekana....
 Jamaa wakisimamia usalama pande hizo wakiwafukuza raia waliokuwa wamekusanyika eneo hilo na kuongoza magari kuondoa foleni eneo hilo.....
 Katapila likiendelea na kazi ya kubomoa hapa ni jengo la pili lililokaribu na Green Acres nalo likiliwa hapa tayari ukuta ukiwa unashushwa.....
Katapila likiendea kusambaratisha kuta hizo..

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger