BUNGE LA TANZANIA LAPITISHA KODI YA KADI ZA SIMU (SIM CARD)

Bunge limepitisha sheria ya fedha inayoanzisha kodi kwenye Kadi ya simu. Kila mwenye Kadi ya simu, bila kujali matumizi yake ya simu, atakuwa analipa tshs 1000 kwa mwezi. 

Kodi hii imeanza tarehe 1 Julai 2013. 

Pendekezo hili la kodi lilitolewa na waziri wa Fedha wakati anasoma hotuba yake ya Bajeti. Lakini kwa mshtuko mkubwa nimejua leo kuwa kodi hii iliingizwa kwenye finance bill na kupitishwa. 

Kwa kodi hii maana yake ni kwamba mwananchi wa kawaida, tuseme mwananchi anayefanya kazi ya kuuza maandazi barabarani kila siku, analipa kwa mwezi tshs 1000 sawa sawa na Mbunge ambaye analipwa tshs 11.2m kwa mwezi kama mshahara bila posho za kukaa, posho ya kujikimu na safari mbalimbali. Mwananchi muuza karanga, atalipa sawa na Bakhresa! 

Kinachonishangaza ni kwamba kuna ukimya mkubwa sana kuhusu kodi hii mpya (labda ziara ya Obama). Kodi hii ni mbaya sana. Very rudimentary. Ingawa wabunge wameipitisha, ni vema wananchi wasimame kukataa.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger