Habari kutoka kwa baadhi ya Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba Mtanzania aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani Japhariameaga dunia kwa kujinyonga.
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo,alisema ” I hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga.
Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha shughuli zote
zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu",alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara.
Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi kimasomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji.
No comments:
Post a Comment