HIVI NDIVYO AUNTY LULU ALIVYOHAHA KUMUONA RAIS OBAMA.

MSANII wa filamu Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ alinaswa akihaha kutafuta mwanya wa kuonana na Rais wa Marekani, Barack Obama muda mchache baada ya kuwasili nchini. Aunty Lulu alinaswa na paparazi wetu maeneo ya Kinondoni, Jumatatu (siku ambayo Obama aliwasili) ambapo alionekana akipiga simu kwa rafiki zake wanaofanya kazi ikulu akiwaomba japo kitambulisho cha kuingia kwenye mkutano aliohutubia rais huyo.
Akizungumza na paparazi wetu Aunty Lulu alisema tangu aliposikia taarifa za ujio wa Obama Tanzania, alifurahi na alikuwa akimuota kila mara kwani huwa akisikia sauti yake akiwa anahutubia anachanganyikiwa ndiyo maana alifanya kila jitihada za kuingia ikulu lakini ilishindikana.
“Jamani serikali ingetuangalia hata sisi jamani tumuone Obama naye atuone sisi wasichana wa Kitanzania tulivyo wazuri, warembo na wakarimu, wageni wengi wakiingia Bongo lazima warudi kwa mara nyingine!” alisema msanii huyo.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger