WACHINA WATUA NCHINI KUWASAKA WAINGIZA MABOMU JIJINI ARUSHA.

WATAALAMU wa mabomu kutoka China, wamewasili nchini kutafuta waagizaji wa bomu la kurushwa kwa mkono, lililorushwa na kuua watu wanne katika uwanja wa Soweto Juni 15, mwaka huu mkoani Arusha.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, akizungumza jana katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), alisema katika jitihada za uchunguzi wa bomu hilo, tayari wataalamu kutoka China, wako mjini Arusha, kutambua taasisi iliyonunua bomu hilo.Bomu hilo lilirushwa katikati ya umati wa watu, wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kikihitimisha kampeni zake za udiwani katika Kata ya Kaloleni, ambapo mbali na kuua watu wanne, watu wengine zaidi ya 70 walijeruhiwa.Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo 
Kabla ya tukio hilo la Soweto, mtu mmoja asiyejulikana alirusha bomu la mkono katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Parokia ya Olasiti, Mei 5 mwaka huu na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 30.
“Milipuko yote miwili inaelekea kufanana lakini bomu la Olasiti, liligundulika limetengenezwa nchini Urusi na namba zake za usajili hazikupatikana. “Lakini hili la Soweto ni tofauti kidogo, namba zake zimepatikana na imegundulika limetengenezwa China na hivyo wataalamu kutoka China wako hapa kwetu wanaendelea kubaini nani aliuziwa kwa sababu huwa yanatengenezwa kwa kufuata namba,” alisema.
Kwa mujibu wa Mulongo, taarifa za awali za makachero wa Polisi nchini, zimebaini kuwa watu waliohusika na milipuko miwili ya mabomu jijini Arusha, walianzia mipango yao jijini humo.
Mulongo alisema ukweli utadhihirika hivi karibuni na kuwataka wananchi kuwa na subira, ili vyombo husika vikamilishe uchunguzi wake.
Alisema Serikali itamchukulia hatua mtu yeyote atakayebainika kuhusika bila kujali cheo chake, kwani mambo hayo ni ya kudhalilisha na kufedhehesha.
Aliwashukuru wakazi wa Arusha waliofika kutoa ushahidi wa watu waliohusika katika tukio la Soweto, na kuongeza kuwa upelelezi unaendelea kwa makini, ili kuepuka kukamata watu wasiohusika.
Aliwataka wanasiasa nchini, kutotumia milipuko hiyo ya mabomu kuwa ajenda za kisiasa, kwa kuwa kufanya hivyo ni kuidhalilisha Tanzania nje ya nchi, na kuipotezea wageni, jambo ambalo linaweza kuipotezea mapato mengi ambayo imekuwa ikiyapata kutokana na utalii

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger