BAADA YA KUPATA UONGOZI WA BONGO MOVIE, DK CHENI ATAKA KUIRUDISHA KAOLE

MWENYEKITI Msaidizi wa Bongo Movie Unity, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’ amesema amekumbuka na kutamani kurudisha Kundi la Sanaa ya Maigizo la Kaole ‘Kaole Sanaa Group’ liwe na nguvu kama zamani.
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’.
Dk. Cheni alisema japo kundi hilo limeonekana kupoteza mvuto wake wa awali, lakini anaamini wasanii wengi wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya filamu kwa sasa wametoka katika kundi hilo maarufu.
Hata hivyo, pamoja na kupotea kwa kundi hilo, Dk. Cheni anatamani sana kulirejesha kwenye ulingo wa sanaa na kwamba kuna mikakati anayoiandaa ili kukamilisha azimia hiyo.
“Naitamani Kaole ya zamani, nahisi kama kuna vionjo vinakosekana siku hizi. Wasanii wengi wenye majina makubwa kwa sasa wametoka kwenye kundi hilo, lakini nitajitahidi kulirudisha, naamini nitafanikiwa,” alisema Dk. Cheni.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger