STAA aliyeliteka soko la mduara kwa kibao chake cha Majanga, Snura
Mushi amesema watu wenye chuki na yeye wamepanga njama za kumshusha
kwenye chati kutokana na maendeleo yake.
Akipiga stori na paparazi wetu juzi, Snura alisema: “Nashangaa sana
ninapofanya jambo zuri halafu watu wanaligeuza kuwa baya ili nichafuke
jina na kunipunguzia mvuto kwa mashabiki wangu.”
Chanzo cha yote ni baada ya mwanadada huyo kupiga shoo kwenye Ukumbi
wa Buliyaga, Temeke, Dar siku chache zilizopita, kundi la watu
wasiojulikana walianza kueneza taarifa kuwa alifanya vibaya na mashabiki
wakamtaka ashuke jukwaani jambo ambalo alisema halikuwa na ukweli
wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment