Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo alisema jengo
hilo lilipaswa kuwa la ghorofa sita na kuamuru kubomolewa kuanzia
ghorofa ya saba kwenda juu.
Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na
mashahidi 13 wa upande wa mashtaka, vielelezo 20 vilivyowasilishwa na
ushahidi wa utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe, upande wa mashtaka
ulithibitisha pasipo shaka mashtaka dhidi ya vigogo hao waliodaiwa
kuruhusu ujenzi wa ghorofa 18.
Hivyo aliwahukumu washtakiwa hao kila mmoja kulipa faini ya
Sh5milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa
lililokuwa likiwakabili. Kila mshtakiwa alilipa kiasi cha Sh15 milioni
mahakamani hapo na kuepuka kifungo.
Baada ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alisema ndani ya kipindi
cha miezi sita baada ya hukumu hiyo kutolewa, Kifungu cha 40, namba 1 na
2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinawaruhusu kutaifisha
jengo hilo.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na Mawakili Majura Magafu na Paschal Kamala.
No comments:
Post a Comment