JESHI la majini la Australia limekamata na kuharibu kilo 353 za
madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani inayokadiriwa kuwa zaidi
ya dola milioni 700 katika pwani ya Tanzania.
Askari wa meli ya HMAS Melbourne waliyagundua madawa hayo katika meli
moja Jumatano iliyopita wakiwa katika shughuli za kupiga vita ugaidi na
kuimarisha usalama maeneo ya baharini Mashariki ya Kati na Bahari ya
Hindi.
Mkuu wa kikosi hicho, Daryl Bates, alisema hatua hiyo ilikuwa ni pigo
katika kukwamisha njia za kupatikana kwa fedha zinazotumiwa na magaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment