MSANII kinda kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rahma Bagenzi ‘Rayuu’
amesema kuwa, kamwe hatokoma kutembea na waume za watu kwa kuwa sheria
ya dini yake ya Kiislamu inamruhusu kuolewa na mume wa mtu.
Akipiga stori na paparazi wetu, Rayuu alisema kipindi cha nyuma
aliwahi kutoka kimapenzi na mume wa mtu (hakumtaja jina) na kufikia
hatua ya kufikishwa polisi na mwenye mke lakini haimaanishi kuwa
hatatembea tena na mume wa mtu.
“Nikila kiapo cha kutotembea na waume za watu nitakuwa naongopa,
kwanza dini yetu imeruhusu ndoa za uke wenza huenda Mungu kaniandikia
niolewe ndoa ya aina hiyo sina uwezo wa kupingana naye,” alisema Rayuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment