MWIGIZAJI wa Bongo Movies, Salim Ahmed ‘Gabo’ amepata ajali mbaya ya gari maeneo ya Kiwalani jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo makini, Gabo aliyekuwa katika gari binafsi, aligongana na gari lingine na kupata jeraha mguuni hivyo kulazimika kulazwa kwa takriban wiki tatu kisha kuruhisiwa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza
na paparazi wetu baada ya kutoka hospitali, Gabo aliyeitendea haki
Sinema ya Majanga ya Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’, alieleza mazingira ya
ajali.
“Nilikuwa
naendeshwa na rafiki yangu lakini ghafla tukagongana uso kwa uso na
gari lingine, nashukuru magari hayakuumia sana lakini mimi nililazwa
kwa wiki tatu kutokana na jeraha nililolipata mguuni,” alisema Gabo.
No comments:
Post a Comment