Katika
watu maarufu hapa Bongo ambao wako very open inapokuja swala zima la
mahusiano, iwe rafiki wa karibu au mpenzi wa moyo, basi jina la Wema
Sepetu liwekwe on top of that list, ni moja kati ya watu ambao hawawezi
kuzuia hisia zake, haijalishi yupo hadhara gani. Tumeona jinsi alivyo
open kuzungumzia siku zote mapenzi yake kwa Diamond Platnumz, hata pale
walipokuwa wameachana, kama ni drunk in love basi basi we muuliza Wema
ni nini haswa maana yake. Basi ukiachana na Diamond Platnum ambaye sasa
ndiye mmiliki halisi wa Diva huyo ambaye ni gumzo katika media
mbalimbali hapa Bongo, hii ndio list ya wanaume ambao waliwahi kubambwa
katika kipindi tofauti wakifaidi mabusu ya Wema Sepetu;
Mwinyi:
Huyu ni rapper maarufu wa Machozi band, inasemekana walishawahi kutoka
pamoja, na mwinyi ndiye aliyewahi kumvalisha pete ya uchumba,tena mbele
ya kadamnasi, akiwa stejini kazini.
Unkown:haikujulikana mapema jina lake halisi, ni mmoja kati ya wanaume waliowahi kubambwa wakifaidi mabusu ya Wema.
Tbway:
jina lake halisi ni Tonny Albert, ni mtangazaji wa kipindi cha 5select
kinachorushwa na EATV, dont get it twisted,hapa Wema alikuwa ana-show tu
love kwa jinsi anavyokubali kazi za huyu presenter maarufu.
Romyjones:
huyu ni Dj na pia ni ndugu yake kabisa Diamond Platnumz, Wema anamuita
Romy shemeji, sidhani kama kuna ubaya wa kumbusu shemeji mara moja moja,
basi hapa Wema naye hakuona noma, kumpa hata busu shemejie.
Martin Kadinda:
akiwa ndiye manager wake Wema Sepetu, pia Martin ni mtu wa karibu sana
wa Wema, mara nyingi huoneka pamoja katika sehemu tofauti, hii moja
ilionekana kule istagram akipozz, huku Martin akimbusu Wema Sepetu,
kishkaji tu.
Chaz Baba:
Enzi hizo za mwalimu, wakati Wema Sepetu akiwa ameshadondoka kimapenzi
kwa Chaz baba, alionekana akijiachia kila apatapo nafasi, hata hivyo
baadae walikuja kuachana, ndipo Diamond Platnumz alipoingia na
kufanikiwa kumficha kabisa mtoto, hadi hii leo.
Credit Vibe
No comments:
Post a Comment