Tangu
Nemanja Vidic alipotangaza rasmi kwamba msimu ujao hatokuwepo Old
Trafford kulianza tetesi juu ya mchezaji gani atapewa nafasi ya kurithi
mikoba ya unahodha ambapo Wayne Rooney mmoja wa wachezaji wakubwa ndani
ya klabu ya Manchester United alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kuwa
nahodha mpya wa United wakati timu hiyo ikiwa chini ya David Moyes.
Baada ya kutimuliwa kwa kocha huyo na
nafasi yake kuchukuliwa na Louis Van Gaal, mshambuliaji wa Uholanzi na
nahodha wa timu ya taifa ya Uholanzi Robin van Persie amekuwa akipewa
nafasi ya kumrithi Vidic, huku Van Gaal akisema kwamba yeye na RVP wana
filosofia moja hivyo wanakuwa na urahisi wa kufanya kazi pamoja kama
kocha na nahodha wake.
Hali hiyo imepelekea Wayne Rooney
ambaye alikuwa akipewa nafasi kubwa ya unahodha msimu ujao kuzungumza
akisema “navutiwa na suala la kuwa nahodha, nimeshawahi kuwa anahodha wa muda United kwa mara kadhaa na kupata jukumu hilo moja kwa moja litakuwa jambo zuri sana.”
Akizungumzia suala la Van Persie kupewa nafasi kubwa ya kuwa nahodha ajaye wa United, Rooney anakwambia ikiwa kocha wetu atamchagua mtu mwingine basi kiukweli kabisa sitokuwa na tatizo na hilo, nitaheshimu maamuzi yake… Robin
ni nahodha wa nchi yake, ameshawahi kuwa nahodha wa Arsenal na ikiwa
atapata nafasi hiyo United basi naamini atafanya kazi nzuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment