Wema Sepetu na jokate mwengelo ni kati ya wasichana warembo
hapa bongo na role models. Wote mwanzo wao ulitokana na mashindano ya
miss Tanzania ya mwaka 2006 ambapo wema sepetu aliibuka mshindi wa
kwanza huku jokate akikamata namba mbili.
Najua huwezi kumuongelea wema sepetu au jokate bila kumuingiza diamond
platnumz kidogo. Mnamo mwaka 2010 hadi 2011 diamond alianza kwanza
kumdate mshindi wa kwanza wa miss tz jokate na kuachana nae na kuamia
kwa mshindi wa pili yaani wema. Je, diamond nae alikua anataka kujibu
swali tunaloliuliza ? na kama amelijibu inabidi kushare jibu ilo na
mashabiki tukajue.
Wema na jokate wote wanafanya movie na vigumu kujua nani zaidi katika
uigizaji wa movie sababu kila mtu anasababu yake ya kumkubali mmoja
wao.Twende kwenye fashion wema na jokate wamekua role models wa warembo
wengi katika swala la uvaaji.
Tukija kwenye Ujasiriamali wema na jokate hawapo nyuma. Wema
alianzisha kampuni yake ya Endless Fame Films ambayo inatengeneza bongo
movies. Pia wema anakipindi chake cha TV kinachoitwa In My Own Shoes
kinachooneshwa na Channel 5 EATV. Tukija kwa Jokate mwengelo kikubwa
kwake ni product ya Kidoti inayompa chati sana ukiachana na kazi ya
utangazaji anayofanya kwenye channelO ya Afrika Kusini.
Hata vibe magazine tuliliona hilo na kuamua kuwaweka wema na jokate
katika cover page wakati ndio kwanza kuna issue tatu tu huku nyingine
ikiwa ni kijana aliyewahi kuwadate wote diamond platnumz.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment