TUNAMALIZIA makala haya ya Sabrina Rupia ‘Cathy’
tuliyoyaanza wiki tatu zilizopita, mwigizaji huyu alifunguka mambo mengi
kuhusiana na maisha yake, bila shaka kupitia mfululizo wa makala haya,
msomaji utakuwa umejifunza vitu vingi kutokana na hatua ambazo amepitia
maishani na leo hapa anafunguka kuhusu anavyofurahia maisha ya ndoa kwa
kuolewa na mume ambaye amemzidi umri SHUKA NAYO…
Mwandishi: Kwa nini ulipenda mumeo akuzidi umri?
Cathy: Kwanza
nilipenda busara zake na namna anavyonilea kama mtu wake wa karibu, si
mtu wa mbwembwe kama walivyo wengine, namfurahia kwa sababu tunafanya
maisha ya kweli, lakini nilitaka kupata mwanaume mwenye huruma ambaye
hatoniumiza kama wafanyavyo vijana kwa sababu ya maisha ambayo
nimeyapitia ya kuwa mpweke baada ya kufiwa na baba yangu.
Mwandishi: Una watoto wangapi kwa sasa?
Cathy: Sipendi kutaja watoto ila fahamu ni mama wa familia.
Mwandishi: Je ndoa uliyonayo ni ya ngapi kwako?
Cathy: (Anatahamaki kidogo) We! Ndoa ya ngapi? Hii niliyonayo ni ya kwanza na mwisho!
Mwandishi: Vipi kuhusu mameneja wako katika kazi za uigizaji hawakusumbui suala la kukusimamia bila kuwapa tunda la mumeo.
Cathy: Hapana najitambua lakini pia najivunia kuwa mme wangu ndiye meneja wangu kwa hiyo tunda ni halali yale kabisa.
Mwandishi: Ni kweli Bongo Muvi hamko tayari kuwatoa wasanii wachanga?
Cathy: Kwa kifupi hela zinaenda kwa wenye hela, hata mimi naweza
kulalamika lakini nikipata nitachukua waliopata wenzangu na kuwaongezea
na wale wapambane kutoka.
Mwandishi: Kwa nini msibebane?
Cathy: Ninachojua cha msingi ni kufaiti unavyojua mwenyewe lakini
usikae kwa kumsubiri flani atoke ili akupe kiki hakuna mtu wa kukufanyia
hivyo.
Mwandishi: Duuh! Kwa hiyo kila msanii anatakiwa kujibeba kivyake?
Cathy: Nafasi huwezi kupewa cha msingi ni kupigana na kutafuta upenyo wa kutoka iwe kwenye muvi au nje ya sanaa.
Mwandishi: Mpaka sasa una filamu ngapi?
Cathy: Kama nne au tano, kuna DNA, Wheel Chair nilifanya na Cloud, Saa Nne, Kaburi na Simu ya Mkononi ambazo hazijatoka.
Mwandishi: Nini ushauri wako?
Cathy: Watu wasibweteka hasa kina dada watumie nguvu zao kufanya kazi
lakini pia wasanii wachanga wafaiti wenyewe wasisubiri kuolewa, kila
mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake.
Mwandishi: Unazungumzije suala la ajira kwa vijana?
Cathy: Wanyanyuke waache uzembe kwani hata kilema anatamani japo
anyanyuke kwa dakika kadhaa ili atembee, asiye na mikono anatamani
angekua nayo ili imsaidie japo kulima sembuse wewe uliyekamilika
unashindwa kujisaidia mpaka usubiri kutolewa!
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment