BIG Boss wa Kampuni ya Five Effect, William Mtitu
amesema amekoma kutumia usafiri wa boti kwani ulimfanya akose amani
juzikati walipokwenda Zanzibar katika Tamasha la Ziff.
Akipiga stori mbili tatu na paparazi wetu, Mtitu alisema alipokuwa
safarini, boti ilimtoa ushamba baada ya hali ya hewa kumshinda na
kutapika sana akiwa humo.
“Boti imenitoaje ushamba yaani nimetapika njia nzima tangu naanza
safari hususan kutoka Zanzibar hadi nilipokaribia kufika Dar ndio
nikaacha kutapika huku nikiwa nimeshikiliwa na Rich na Barafu, sipandi
tena aisee,” alisema Mtitu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment