Mamlaka nchini Australia imetoa tahadhari dhidi ya matumizi ya charger
aina ya USB feki au zilizo chini ya viwango huku zikiwa zimechomekwa
kwenye umeme baada ya mwanamke mmoja kufariki dunia wakati akitumia
charger ya aina hiyo kucharge simu yake iliyokuwa imechomekwa kwenye kompyuta yake ndogo.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 28 alikutwa amevaa headphones masikioni akiwa na
kompyuta yake mikononi huku akiwa na majeraha ya kuungua kifuani na masikioni nyumbani kwake huko Gosford, Kaskazini mwa Sydney.
Polisi nchini humo bado wanafanya uchunguzi kujua mazingira ya kifo
hicho lakini kitengo cha biashara kilichofuatilia suala hilo
kimetahadharisha kuwa charger za simu zilizo chini ya viwango ni moja ya
sababu kubwa.
Mwanamke huyo ambaye ripoti zinadai kuwa anatokea nchini Ufilipino na
baadae kuwa raia wa Australia alivaa headphones zilizokuwa zimechomekwa
kwenye kompyuta ndogo iliyokuwa imechomekwa kwenye socket ya umeme.
No comments:
Post a Comment