HII NDIO LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA WATU ZIKO HAPA...ANGALIA PICHA ZOTE YALIYOJIRI USIKU WA JANA HAPA

Millard Ayo.
Mtangazaji maarufu Salim Kikeke wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC ametwaa taji la Mtangazaji wa Runinga Anayependwa katika toleo la kwanza la Tuzo za Watu za Tanzania au Tanzania People’s Choice Awards katika sherehe zilizofanyika Serena Hotel, Ijumaa jijini Dar Es Salaam.
Vipengele 11 (kumi na kimoja) vilikuwa vikishindaniwa. Mshindi katika kila kipengele ameibuka na zawadi ya shilingi milioni moja pamoja na tuzo. Chini ya orodha ni picha za tukio hilo.

ORODHA YA WASHINDI
1. MTANGAZAJI WA REDIO ANAYEPENDWA
Millard Ayo – Clouds FM
2. KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA
Amplifaya – Clouds FM
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA
Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA
Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA
Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA
Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME
My Number One – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE
Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA
Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA
Ndoa Yangu
Salim Kikeke - BBC Swahili
Salim Kikeke wa BBC Dira ya Dunia, mshindi wa kipengele cha Mtangazaji wa Runinga Anayependwa, akizungumza machache baada ya kutangazwa.
4K0A3518
Mkongwe King Majuto akiwapa mashabiki wake heko kwa kumpigia kura. Ameshinda kipengele cha Muigizaji wa Kiume Anayependwa Kwenye Filamu. Pembeni ni Lulu Michael, mshindi wa Mwigizaji wa Kike Kwenye Filamu Anayependwa.
4K0A3607
Picha ya pamoja ya walionufaika katika Tuzo za Watu mjini Dar Es Salaam, Juni 27, 2014.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger