ULOZI! Katika hali ya kushangaza, mama aliyetajwa
kwa jina la Khadija Omari amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya
kushikana uchawi na kikongwe anayefahamika kwa jina moja la Siberi akiwa
na mganga wake, Rashid na kuibua timbwili lililotikisa, akimtuhumu
kikongwe huyo kumchukua mwanaye kimazingara ‘msukule’.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita maeneo ya Mgeni-Nani, Mbagala
jijini Dar na kusababisha sekeseke kubwa lililofunga mtaa kufuatia
mvutano ulioibuka baina ya wakazi wa mtaa huo huku baadhi wakiamini
ushirikina wakimhusisha kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa Khadija ambaye ni mama mzazi wa mtoto anayedaiwa
kuchukuliwa msukule aitwaye Tausi, mwanaye huyo alifariki dunia Agosti,
mwaka jana katika mazingira ya kutatanisha.
Alisema kifo cha mwanaye
kilimtatiza hivyo alikwenda kwa waganga wa jadi ‘kuchungulia’ kama
alifariki dunia kweli au ni mauzauza ndipo akabaini kuwa kikongwe huyo
ambaye alikuwa mwenye nyumba wake anahusika.
Kufuatia hali hiyo, Khadija aliamua kuondoka kwenye nyumba ya
kikongwe huyo kwani alikuwa akikutana na mauzauza kila kukicha na
kutimkia mkoani Mwanza huku akijipanga kutafuta mtaalam wa kumtoa
mwanaye alipowekwa msukule.
Alisema hivi karibuni alirejea Dar na kutinga kwa kikongwe huyo akiwa na waganga wa jadi ili kumpata mwanaye.
Hata hivyo, zoezi hilo halikufanikiwa baada ya ndugu wa kikongwe huyo
kuingilia kati na kuanzisha timbwili la aina yake wakimtetea kwa madai
hawana imani kama anajihusisha na vitendo vya aina hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment