MASTAA WAPIGWA CHINI NA MILLARD AYO

AMETISHA! Prizenta wa Clouds FM, kupitia kipindi chake cha Amplifaya, Millard Ayo amewapiga chini mastaa kibao baada ya kutwaa Tuzo ya Mtangazaji Anayependwa wa Redio na nyingine ya Kipindi cha Redio Kinachopendwa yaani Amplifaya katika Tuzo za Watu.
Prizenta wa Clouds FM, kupitia kipindi chake cha Amplifaya, Millard Ayo (wa tatu kushoto) akiwa na tuzo pamoja na wenzake.
Mpango mzima ulichukua nafasi usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita ndani ya Ukumbi wa Serena Hotel, Posta jijini Dar ambapo Millard aliibuka kidedea kwenye kategori hizo mbili na kuwafunika baadhi ya mastaa aliokuwa akigombea nao.
Wengine waliotwaa tuzo ni pamoja na Salama Jabir, Diamond Platnumz, Mzee Majuto, Lulu, Salim Kikeke, Nisher na wengine.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger