MSANII nguli katika soko la filamu Bongo, Lucy
Francis Komba amefunguka kuwa yeye ni zao mojawapo la hayati George
Otieno Okumu ‘Tyson’.
“Mimi ni zao la Tyson, nimeanzia katika mchezo wa maigizo wa Mambo
hayo uliokuwa ukirushwa katika Kituo cha Runinga cha ITV na ndiyo ukawa
mwanzo wangu kujulikana, asingekuwa yeye sijui ningekuwa wapi,
nitazidi kumuombea ili Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi,” alisema Lucy.
Tyson aliyefariki kwa ajali ya gari wiki moja iliyopita mkoani Morogoro
na kusafirishwa nyumbani kwao Kenya, anatarajiwa kuzikwa Jumamosi hii
huko Kisumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment