HATIMAYE staa wa sanaa za maigizo Bongo, marehemu
Said Ngamba ‘Mzee Small’ amezikwa juzi Jumatatu katika Makaburi ya
Segerea jijini Dar es Salaam, Risasi Mchanganyiko lilikuwepo msibani
hatua kwa hatua.
Msiba huo ulihudhuriwa na mamia ya watu akiwemo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Jakaya Kikwete na ujumbe wake kutoka
Ikulu, mastaa mbalimbali na wadau wengine wa filamu.
BONGO MUVI WAJITOKEZA
Awali, ilionekana kuwepo
harufu ya wasanii wa Bongo Movies Unity kutohudhuria baada ya
kutoonekana msibani hapo tangu siku ya msiba na mkesha wa kuamkia siku
ya mazishi.
Wasanii walioonekana mstari wa mbele walikuwa ni wale wa vichekesho
wakiongozwa na Habib Mrisho ‘Sumaku’, Hemed Maliyaga ‘Mkwere’, Jumanne
Shabaan ‘Matata’ na wengineo huku wasanii wa filamu wakiwa wa kuhesabu.
Mpaka Jumapili usiku, wasanii wa filamu walioonekana nyumbani kwa
marehemu Mzee Small walikuwa ni Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’, Wastara Juma
na Simon Mwakifwamba ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania
‘TAFF’.
MASTAA WAMGOMBEA JK
Rais Kikwete aliingia
msibani hapo na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais wa TAFF, Mwakifwamba
kisha kusalimiana na watu waliokuwepo msibani ambapo wasanii walionekana
kumgombea JK ili washikane naye mkono.
Akizungumza baada ya kushikana mkono na JK, mmoja wa wasanii wa Bongo
Muvi ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alisema: “Ni bahati ya
mtende kushikana mkono na rais ndiyo maana hakuna aliyekuwa tayari
kuipoteza.”
WAKONGWE
Mbali na mzee Olotu, wakongwe wengine
walioonekana msibani hapo ni pamoja na Mashaka, Mbembe, Mohammed
Fungafunga ‘Jengua’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Hashim Kambi
‘Ramsey’ na wengine wengi.
Timu ya Risasi Mchanganyiko inatoa pole kwa wafiwa wote, ndugu jamaa
na marafiki. Mungu awape wepesi katika kipindi hiki kigumu cha mpito.
Inshaalah!
Innalillah Wain illah Rajiun.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment