Akizungumza kwa masikitiko makubwa na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Rukia alisema alimzaa Hussein mwaka 2008 huko Kilwa lakini katika kukua imekuwa ni tatizo kubwa ambalo linaambatana na kushindwa kuongea wala kukaa.
“Hapa unapomuona anasikia kila kitu, anajua kila unachomuuliza lakini hawezi kukaa wala kuongea. Muda mrefu nampakata au analala tu,” alisema mwanamke huyo.
Mtoto Hussein Jumbe akiwa na mama yake mzazi, Rukia Twalibu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Alisema baada ya mwanaye huyo kufikisha miaka miwili, baba yake mzazi
alitoweka katika mazingira ya kutatanisha hadi sasa hajulikani alipo
kitu ambacho kimempa wakati mgumu sana.Akaendelea: “Nilipobaini hali hii ya mtoto na sina msaada, nilikwenda Hospitali ya CCBRT (jijini Dar) lakini madaktari wa hospitali hiyo walisema ukubwa wa tatizo la mwanangu hawawezi kufanya chochote.
“Juni 22, mwaka huu ndiyo nilikuja hapa Muhimbili ambapo mwanangu anachunguzwa kisa cha kutokua kama watoto wengine ilhali umri unakwenda, bado madaktari hawajaniambia chochote, naamini wanaumiza kichwa kujua tatizo.
“Hadi kufika hapa Muhimbili nimepata michango kwa watu pia nilipata barua kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi ambayo ilinisaidia kupata kiasi kadhaa cha pesa,” alisema mama huyo.
Rukia na mwanaye amelazwa katika Wodi ‘A’ ya Watoto, kwa aliyeguswa na tatizo la mtoto Hussein, awasiliane na mama yake kwa namba 0714 177 071.
Naamini ukimsaidia mtoto huyo, utapata baraka katika kila ukifanyacho.
No comments:
Post a Comment