MADUKA wawili ya wafanyabiashara wa katika mji mdogo wa Buseresere katika wilaya ya Chato mkoani Geita yameteketea kwa moto na kuunguza mali ambayo inadaiwa kuwa ni zaidi ya shilingi milioni mia moja.
Tukio
hilo limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 10 na nusu usiku
katika mtaa wa msikitini na kuteketeza mali za wafanya biashara wawili.
Katika tukio hilo familia moja ya Yahaya Runwa imenusurika kuteketea kwa moto huo.
Runwa alieleza kuwa usiku alisikia mlipuko mkubwa nje kwenye vibanda vya biashara alivyowapangisha wafanyabiashara
hao na alipotoka nje alikuta mtungi wa gesi umelipuka na unawaka moto
na aliporudu ndani hari ilikuwa mbaya zaidi ndipo akaanza kupiga kelele
za kuomba msaada kwa wananchi.
Akizungumza
na waandishi wa habari afisa mtendaji wa kata hiyo Daudi Ruhangija
alisema chanzo cha moto huo kuwa ni hitilafu ya umeme uliokuwa umeunganishwa kinyemela katika nyumba hiyo.
Ruhangija aliwataja waathirika hao kuwa ni Faridu Abdul ambaye ni mfanya biashara wa sipea za magari na pikipiki na mwingine ni Maiko Hamko ambaye ni mfanya biashara wa mitungi ya gesi na wote ni wakazi wa mji huo.
Kaimu
kamanda wa zima moto mkoani hapa Hamidu Ngiya alisema baada ya kupata
taarifa kuhusu tukio hilo kutoka kwa afisa mtendaji wa kata walifika
kwenye eneo la tukio wakiwa na gari lenye namba FT3HGA10034 na
kufanikiwa kuzima moto kwa kushirikiana na wananchi waliowakuta kwenye
eneo la tukio.
Hata
hivyo baadhi ya changamoto alizoelezea Hamidu katika kutekeleza zoezi
hilo ni pamoja na uhaba wa vitendea kazi ikiwemo gari moja mkoa
mzima,umbali wa maji ya kuzimia,na uchache wa wafanyakazi ambapo wapo
wanane wakati,vilevile ukosefu wa unifomu wanapokuwa kazini ili waweze
kutambulika kwa urahisi.
Aidha
aliwataka wananchi waache tabia ya kujiunganishia umeme kwa njia ambazo
siyo rasmi kwani kwa kufanya hivyo itakuwa ni kuhatarisha maisha ya
wananchi.
No comments:
Post a Comment