Sofia Nsoba
mkazi wa Manzese - Uzuri jijini Dar es Salaam yuko katika mateso mazito
kwa mwaka wa nne sasa baada ya kugundulika kuwa ana kansa ya matiti.
Akisimulia mkasa huo wa kusikitisha, Bi. Sofia ambaye ana jukumu la
kulea watoto wanne alisema, kwa sasa hali yake imezidi kuwa mbaya zaidi
hadi kufikia titi lake kuoza huku lingine likianza kuathirika na ugonjwa
huo.“Niligundua tatizo langu kwa mara ya kwanza mwaka 2011. Nilikwenda kupima Hospitali ya Aga Khan baada ya kusikia kuna vipimo vya kansa ambavyo vilikuwa vikitolewa bure,” alisema na kuongeza:
“Nilivyogundulika na tatizo hilo nilijitahidi sana na matibabu kwa pesa zangu za kuungaunga lakini mwisho wa siku niliambiwa natakiwa ziwa likatwe kwa kuwa tatizo lilizidi kukua siku hadi siku. Kwa kweli sikuwa na la kufanya, maana uwezo sina na hivi sasa tatizo limeanza kuenea na ziwa langu la kulia.”
Akaongeza: “Naumia sana kuona thamani ya uanamke wangu inapotea maana huenda nikakatwa maziwa yote mawili, lakini ni bora nikubaliane na hilo nipate uzima. Gharama ya matibabu yake nimeambiwa na madaktari si chini ya shilingi milioni tatu kwa matiti yote mawili katika Hospitali ya Muhimbili.
“Naombeni huruma yenu Watanzania wenzangu, sina msaada wowote, mume wangu amenitelekeza na watoto, amekwenda kuoa kijijini. Naombeni msaada wenu ili nifanyiwe upasuaji.”
Kama umeguswa na kisa cha huyo, tafadhali toa msaada wako wa hali na mali kupitia namba 0716780472 au 0752583531. Mjaribu Mungu kwa kuwasidia wahitaji, naye atakufanyia mambo makuu ya kushangaza.
No comments:
Post a Comment