MWANADADA kutoka kiwanda cha Filamu Bongo, Salma
Jabu ‘Nisha’ amewabwatukia wasanii wenzake wanaomshutumu kwamba anatumia
ndumba na kuwataka waache maneno hayo.
Nisha aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kuzagaa kwa tetesi kuwa
alizomewa na wasanii wenzake wakimwita mchawi kutokana na mafanikio
aliyoyapata kwa haraka kwenye sanaa, tofauti na wasanii wengine
wanaosota kwa muda mrefu mpaka kupata mafanikio.
“Unajua siku zote mti wenye matunda ndiyo huwa unapigwa mawe, kipindi
nikiwa bado sijaweza kucheza filamu zangu, yaani nikiwa chipukizi
hakuna aliyekuwa ananizungumzia lakini sasa hivi wananiongelea kila
kona, anayesema mimi ni mchawi basi huwa tunawanga pamoja, mimi
namwamini Mungu sijui na siamini katika uchawi, mafanikio yangu ni Mungu
tu na kujituma kwa bidii,” alisema Nisha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment