Katika segment ya KITENGO, leo katika Kipindi cha Planet Bongo Kinachorushwa EATV: Host Abdallah Ambua Alimtembelea Msanii Wa Muziki wa B'flava, Ally Salehe Kiba, nyumbani kwao anapoishi yeye na familia yake kwa ujumla::Nilikuwa na shauku ya kusikia nini ambacho Ally K angekizungumza kuhusiana na Muziki wake kwa ujumla na hii ''Backwardness'' yake licha ya kuwa msanii mkubwa na anayependwa zaidi Bongo;
After Interview Nilijifunza vitu vifuatavyo:
Kitu cha kwanza ambacho kilinishtua ni Kuona Setup ya Location ambayo waliichagua kufanyia Interview, Lazima niseme wazi haikuwa Kwa Hadhi yake - Hata kama ni usimple, that was too much...
Kwa ufupi ilikuwa ni Unprofessional !! Walikaa on a rough and shabby set mpaka nikawa naichungulia mara mbili mbili.
Kingine ni the way anavyojichukulia: Ni mtu ambae anaonesha kama ndoto zake zote kimuziki zimeshatimia, Especially kufanya kazi na msanii mkubwa duniani , R kelly: He sounded like Nani kama mimi in Tz... HAKUNA !Pia; Namna alivyokuwa anazungumza na kujibu maswali, Haonekani kuwa na strategy zozote za kuukuza Muziki wake na kufanya kitu ambacho mashabiki wake wengi wanakitarajia Aidha ni kwa kutopenda kuanika mambo yake (maybe) lakini as an artist hakuwa na ile promising attitude..
Mengineyo: Hakuvaa vizuri, Hakuwa na ile starlook kabisa, He looked more of An Undergroundartist:
My Take: Inakatisha tamaa kuwa mshabiki wa msanii ambae hana hata dalili za kukata kiu yako kama mshabiki. Ni kwa vile anajua kwamba we are addicted to his music au ni nini?
Ifikie hatua mshkaji ajiongeze kidogo, Music is Business, Na luckily he's on a high demand, Ningefurahi kama angejikagua tena na kufanya kitu ambacho shabiki zake wanapenda.Nisingependa kumtaja; Lakini Diamond is a nice mirror to look at : Sio dhambi Kuiga vitu vizuri.
NAISAPOTI..................... .......
#BringBackOurArtistCampaigne
#ALLYKIBA
No comments:
Post a Comment