Karibu kila mwaka kumekuwa na malalamiko ya wasanii kuhusu kuibiwa
nyimbo au idea za nyimbo zao na Mkali wa Ngololo Style, Diamond
Platinumz, madai ambayo huzua hisia tofauti kwa watu wengi.
Hivi karibuni, mshiriki wa BSS Wababa naye alijitokeza na kudai kuwa
Diamond amemuibia wimbo wake wa Kitorondo na kwamba baadae aliubadilisha
jina na kuuita MdogoMdogo.
Diamond amezitolea majibu tuhuma hizo jana (June 25) wakati akifanya
mahojiano na Jabir Saleh katika kipindi cha The Jump Offf cha 100.5
Times Fm. “Unapokuwa mkubwa sana kunakuwa kuna faida yake na madhara
yake. Na madhara yake yalivyo, unapokuwa mkubwa sana kitu ambacho hakina
maana watu wanajaribu kukifanya kuwa na maana, either kionekane kizuri
au kibaya.”Amesema Diamond. Mfano nilipotoa Moyo wangu nyimbo nyingi
sana zilitoka zinaitwa Moyo Wangu. Lakini hujawahi kusikia hata siku
moja nikasema kuna mtu kaniibia. Kwa sababu lile ni neno ambalo wewe
unavyojua wewe na mimi nikatumia ninavyojua mimi kwa sababu hakuna
mwenye maneno yake duniani.” Alifafanua.
Akizungumzia tuhuma zilizotolewa na msanii Wababa hivi karibuni kuwa
alimuibia wimbo wake wa Kitorondo na baadae akaubadili kuwa Mdogo Mdogo,
Diamond amesema huo ni wimbo wa Asili ambao ulikuwa unaimbwa na bendi
ya Tandale Modern Taarabu, na pia ni ngoma ya mdundiko wa zamani.
“Sitaki niongee kwa sababu nitampa Kick…anyways nilisikia kuna mtu
anasema eti hii nyimbo yangu ya MdogoMdogo kuna mtu kaibiwa kwa neno la
Kitorondo. Sasa mimi nikuadithie story fupi...mimi nimezaliwa Tandale
nimekulia Tandale, kuna bendi ilikuwa inaitwa Tandale Modern Taarab
nyimbo yao ya kwanza inaitwa Tandale (anaimba kidogo). Ukiacha hivyo,
Kitorondo ni jina ambalo ni ngoma ambayo wanaimba hivyo (anaimba). Yaani
hii ni nyimbo.“ Kuna msanii kaichukua kaiimba kama ilivyoile nyimbo ya
mdundiko. Halafu baada ya kusikia neno la Kitorondo kwenye nyimbo yangu
akasema yeye kaibiwa nyimbo. Mimi nimepata taarifa nikasema ana akili
kweli. Yeye ndio kaenda kuiba. Mimi nimetumia neno la Kitorondo kwa
taaluma zangu za kimuziki naliingiza kwa namna gani kama neno, yeye
anasema nimemuibia yeye. Sikujisikia vizuri…halafu nikaulizwa kila
sehemu nikienda nawaambia msiniulize maswalir hayo kabisa.”
Diamond alizungumzia masuala mengi ikiwa ni pamoja na maandalizi ya Tuzo
za BET ambapo anategemea kuwa na mkutano wa kimataifa kwa ajili ya tuzo
hizo huko Marekani, mkutano utakaowajumuisha wasanii wengi wa kimataifa
kama project ya dunia nzima.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment