SNURA AFUNGUKA KUHUSU RUSHWA YA NGONO

Msanii  wa  muziki  na  filamu  Snura  Mushi  amebainisha  kuwa  rushwa  ya  ngono  kwa  wanawake  ni  kikwazo  kikubwa  kinachowakwamisha  wanawake  kutimiza  ndoto  zao...

Snura  aliamua  kungukia  suala  hilo  ili  kuwatetea  wanawake  wanaoombwa  rushwa  ya  ngono  ili  kupewa  kazi, kwa  kusema  ni  kitendo  cha  kinyama  kwani  wengi  wanakuwa  ombaomba  kwa  sababu  tayari  wamekosa  kazi  kutokana  na  kulazimishwa  kitendo  hicho.....

"Wanawake  wanaweza  lakini  wengi  wanakatishwa  tamaa  na  baadhi  ya  watu  wanaotumia  nafasi  zao  vibaya. Unakuta  mwanamke  kafanya  vizuri  na  ana  uwezo  mkubwa  lakini  suala  la  rushwa  ya  ngono  ndo  linalowavunja  nguvu  na  kujikuta  wakiwa  tegemezi  katika  maisha  yao," alisema Snura.

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger