MADEREVA WA MABASI KUTOKA KAHAMA KWENDA MIKOANI KUPITIA SINGIDA WAGOMA, ABIRIA WATESEKA

Hali ilivyokuwa katika mgomo huo abiria wakiwa wamejaa stendi ya mabasi Kahama bila kujua hatma yao
Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Wilayani Kahama mkoani Shinyanga limefanikiwa kuzuia mgomo wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani ambao wanapinga kutozwa faini isiyohalali na Kufanyiwa udhalilishaji na baadhi ya Askari wa kitengo hicho.

Mabasi yanayosafirisha Abiria Kutoka kahama kwenda mikoani leo yamegoma kusafirisha abiria wakishinikiza serikali kuingilia kati suala la faini wanazotozwa na askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama Barabarani.

kwa mujibu wa farajimfinanga.com ni kuwa imefika eneo la kituo kikuu cha mabasi mjini Kahama majira ya saa 12.30 asubuhi na kukuta mgomo huo ukiendela huku madereva wakiwa hawapo katika mabasi yao hali iliyosababisha kuwepo kwa msongamano.
 
Kaimu mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga akiwa na maafisa wengine wa kikosi cha usalama barabarani pamoja na waandishi wa Habari
Kwa mujibu wa Madereva ambao hawakutaka kutaja majina yao wamedai, wamekuwa wakipigwa faini na askari wa mkoa wa Singida na huwalazimisha kulipa faini kubwa ya zaidi ya Shilingi 200,000 huku stakabadhi ikiandikwa shilingi 30,000 inayotambulika serikalini.

Wamesema pia wamekuwa wakilazimishwa kupigwa picha mbele ya mabasi yao wanapokamatwa hata kama wanaendesha mwendo mdogo na kwamba hubambikiziwa kesi, na  baadhi ya madereva wamefikishwa mahakamani kwa kubambikiziwa makosa pale wanapogoma kutoa faini.

Aidha wanapinga kitendo cha ukatili alichofanyiwa dereva Mwenzao wa basi la Princess Munaa Lenye No. T 183 CRW ambaye alivunjwa mkono na askari wa kitengo hicho huko Mbezi Jijini Dar es Salaam baada ya kugoma kunyang’anywa leseni yake.

Hata hivyo mgomo huo ulioanza saa kumi na mbili  Asubuhi umedumu kwa takribani saa mbili na baadaye kuanza kwa safari, huku ikielezwa kwamba mgomo huo ulikuwa ni siri ya Madereva kwani Mawakala wanaokata tiketi hawakuwa na taarifa.

Akizungumza wakati wa mgomo huo Kaimu mkuu wa kitengo cha usalama Barabarani Wilayani kahama Thomas Myonga aliwataka madereva kuendelea na safari zao kwani mgomo huo ni batili na wanaweza kuzisababishia kapuni zao hasara kubwa endapo abiria watafungua Mashitaka mahakamani.

Amewataka madereva kufuata sheria za kudai haki zao ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sehemu zinazohusika ili masula yao yashughulikiwe pasipo kuleta athari yoyote.

Mgomo huo wa madereva wa mabasi umefanyika katika Miji ya Kahama, Bukoba, Mwanza, Msoma na Dar es Salaam huku taarifa zikisema licha ya mgomo huo kumalizika ila kwa sasa maderewa wanaendesha kwa mwendo wa chini kupita kiasi na kwa msongamano, hali inayozidi kuwachelewesha abiria.
Askari polisi wakiangalia hali ya usalama wa abiria kufuatia mgomo huo

Abiria wakiendelea kutawanyika huku mgomo ukiendelea
Abiria wakiwa bado katika hali ya Taharuki
Mgomo ukiendelea

Afande Toma akizungumza na abiria pamoja na Madereva mara baada ya suluhu ya mgomo kupatikana
Mabasi yakianza kuelekezwa kutoka stand na kuanza safari
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani
Mabasi yakiendelea kuondoka kuelekea mikoani

No comments:

Post a Comment

 
Support : WELCOME AGAIN MDADISI
Copyright © 2011. MDADISI WA MAMBO
THIS IS MDADISI
Proudly powered by Blogger