Ndugu
Peter Mashiku anahitaji msaada wa matibabu ya haraka baada ya kuvimba
mkono wa kushoto kwa muda mrefu kutokana na pete alizokuwa amejaa
Ndugu Peter
Mashiku mkazi wa Mwatulole mjini hapa anahitaji msaada wa matibabu ya
haraka baada ya kuvimba mkono wa kushoto kwa muda mrefu, sasa (kama
anavyoonekana pichani)
Hali hiyo imesababisha bwana mashiku aishi
kwenye mazingira magumu kutokana na familia yake kumtenga baada ya kuona
vidole na kiganja kinazidi kuvimba siku hadi siku hivyo inamlazimu mtu
huyo aishi kwa kudra za Mungu na wasamalia wema huku tatizo likizidi
kila siku.
Wakiongea na gazeti hili, wakaazi wa maeneo
hayo walisema chanzo cha tatizo hilo ni bwana huyo kuvaa pete zaidi ya
tatu kama sehemu ya urembo, jirani mmoja wa karibu ambaye hakutaka jina
liandikwe gazetini
“Tunashangaa hata sisi kwani kufuatana na
ucheshi, ukarimu na kulea familia kwanza tulichukua kama mzaha kuona
mwenzetu anavaa pete nyingi, baada ya wiki mkono ulianza kuvimba sehemu
za vidole “Alisema jirani huyo.
Madaktari wa hospitali ya wilaya hii
walisema kwa hatua aliyofikia anahitai msaada mkubwa kifedha ili apate
vipimo vya juu katika hospitali kubwa. Waliongeza kuwa pete hizo hivi
sasa zinaanza kumuathiri kwa kukata sehemu kadhaa na kama jitihada za
makusudi hazitachukuliwa na wasamalia wema huenda hali ikawa mbaya
zaidi.
Kwa mujibu wa daktari wa magonjwa ya msongo
wa mawazo (saikolojia) Hellen Eric alisema mtu huyo anaonekana kama ana
wazimu, lakini vipimo vinaonyesha hali hiyo inatokana na wingi wa vitu
anavyofikiria kuhusu maisha yake.
“Akisaidiwa atarudia hali yake kama mwanzo kwani sio kichaa”
“Akisaidiwa atarudia hali yake kama mwanzo kwani sio kichaa”
Kwa hivyo kutokana na familia yake kusambaratika na wengine kuwa na hali duni anayetaka kumsaidia mawasilianao 0765 866264
No comments:
Post a Comment