WAKATI jana, Julai 9, 2014 George Otieno Okumu
‘Tyson ametimiza siku 40 tangu kifo chake kilichotokea kwa ajali mbaya
ya gari mkoani Dodoma, mama mzazi wa marehemu, Gladys Okumu ameripotiwa
kuugua ghafla nchini Kenya anakoishi.
Mama Tyosn amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan University iliyopo
jijini Nairobi nchini humo kwa kile kilichoelezwa na madaktari kwamba
anasumbuliwa na presha ya kushuka. Akizungumza na gazeti hili juzi
jijini Dar, ndugu wa karibu wa marehemu Tyson ambaye aliomba jina lake
lisiandikwe gazetini kwa sababu si msemaji wa familia, alisema tangu
kifo cha mwanaye, mama huyo amekuwa akisumbuliwa na presha hiyo.
“Kifupi tangu George (Tyson) amefariki dunia mama hayuko vizuri
kiafya. Juzi (Jumapili) alizidiwa akakimbizwa Hospitali ya Aga Khan na
kulazwa.
“Kikubwa ambacho naamini kimekuwa kikimsababishia tatizo hilo ni kitendo cha kutopewa undani wa ajali iliyomuua Tyson.
“Yaani alichoambiwa yeye ni kuwa, mwanaye amefariki kwa ajali ya
gari. Sasa ilikuwaje, wapi, walikuwa wangapi, wangapi walipona, walikuwa
wakitokea wapi kwenda wapi? Hajawahi kuambiwa,” alisema ndugu huyo.
Naye ndugu mwingine wa marehemu Tyson aliye jijini Nairobi
alipozungumza na gazeti hili juzi kwa njia ya simu, alikiri mama huyo
kusumbuliwa na presha na kulazwa.
Tyson alifariki dunia Mei 30, 2014 katika ajali mbaya ya gari aina ya
Toyota Noah iliyotokea eneo la Gairo akitoka Dodoma mjini na wenzake
watano ambao walinusurika kifo kwa kujeruhiwa na kutibiwa. Alizikwa Juni
14, mwaka huu kwenye Kijiji cha Siaya, Kisumu, Kenya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment