MWIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Yobnesh Yusuf
‘Batuli’ ametamka kuwa hakubaliani kabisa na wale mastaa wenye tabia za
kufuturisha watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi.
Akizungumza na paparazi wetu, Batuli alisema anaamini kwamba twawabu
nzuri zinapatikana kwa kufuturisha watu wenye mahitaji kama watoto
yatima na ndiyo maana yeye amejiandaa kuwafuturisha.
“Wasanii tubadilike, tuwafuturishe watu wenye mahitaji ili kuwafanya
na wao wafurahi, banafsi nitafanya hivyo mwezi huu, nitafuturu na
wasiojiweza,” alisema Batuli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment