AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26),
mkazi wa Sinza ya Kwaremmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za
utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.
Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzikati kwa sauti ya kukata
tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya
Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.
’’Baada ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti
kwenye mguu wa kulia. Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na
baada ya muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda
kilikuwa kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
“Mwanzoni mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi
unatoka sehemu mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana
umeoza tena una matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi
kukaa jirani na mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.
Peter alisema atashukuru kama atapata nauli ya kurudi kwao,
Makambako, Njombe kwa vile ameona maisha magumu huku akiishi kwa
kushindwa kula na kulala kwa shida.
“Ila namshukuru sana msamaria mwema anaitwa Louis, ndiye anayenisaidia kwa sasa,” alisema.
Aliongeza kuwa, baada ya kuhangaika kusaka nauli bila mafanikio, baadhi
ya watu walimwambia atoe taarifa kwenye Magazeti Pendwa ya Global
Publishers ambayo yanasomwa na watu wengi Tanzania, atasaidiwa.
“Napenda kuwaomba Watanzania mnaosoma Magazeti Pendwa ya Shigongo
mnichangie pesa ili nipate matibabu na nauli ya kurudi kwetu. Wenye
kukuguswa na tatizo langu wanaweza kunisaidia kwa kutumia namba ya simu
0716 122 780, Louis.”
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment